
Ushauri huwo umetolewa na meneja wa mamlaka ya hali ya Hewa Pemba Bishara Rashid Mdoe huko katika viwanja vya maonesho chamnangwe Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema ili wakulima waendelee kupata mavuno mazuri nilazima wabadilike kutoka kile kilimo ambacho niche asili na badalayake wajikite zaidi katika kilimo ambacho kinafuata miongo ambayo inatangazwa na mamlaka husika.
Aidha amewataka wananchi kufuatilia utabiri wa hali ya hewa unao tolewa ili kuendana na mazingira na kuepuka majanga yanayoweza kuepukika.
Hatahivyo ameto wito kwa wananchi kufika katika maonyesho iliwapate kujifunza zaidi na kuwa walimu wazuri wabaadae.
Comments