
Akizungumza huko Fuoni Mambosasa mara baada ya
kuikagua na kukabidhi Mhe.Kheir amesema ujenzi wa barabara hiyo ni utekelezaji
wa ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshmiwa
Dk.Ali Mohamed Shein katika uimarishaji wa barabara za
ndani.
Amesema kumalizika
kwa Barabara hiyo kutapelekea kuimarika kwa mawasiliano ya usafiri wa barabara
hususani kwa wananchi wa maeneo ya Fuoni Mambosasa na Mwera meli sita.
"Kutengenezwa
kwa barabara hii ni utekelezaji wa ahadi ya Mhe Rais kwa kuimarisha barabara za
ndani na itaunganisha mawasiliano ya barabara kwa wananchi wa maeneo haya
itakayounganisha barabara ya Fuoni Mambosasa na Mwera meli sita " (Alisema
Mhe.Kheir).
Aidha Mhe Haji
amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara ya nchi itaendelea
kuimarisha miundombinu ya barabara za ndani katika maeneo mbali mbali ya
zanzibar ili kuinua uchumi wa wananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Hata hivyo waziri
Kheir amewapongeza wananchi wa maeneo itakayopita barabara hiyo kwa kujitolea
kuondosha vipando vyao na sehemu ya majengo ya makaazi yao na kuridhia
kufanyika ujenzi wa barabara hiyo.
"Nitumie nafasi
hii kuwashukuru wananchi wa maeneo haya kwa kuunga mkono juhudi za Serikali
katika kuwapelekea karibu wananchi wake huduma za kijamii kwa kukubali kutoa
maeneo yao na kutekelezwa kwa mradi huo" alisema Mhe Haji .
Mapema akizungumza
katika zoezi hilo injinia Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Ali Omar Ali amesema barabara hiyo
yenye urefu wa kilomita 3.4 ya Fuoni Mabosasa hadi Mwera meli sita itagharimu
jumla ya billioni 3.59 itajengwa kwa kiwango cha lami.
Amesema hakuna fidia
itakayotolewa kufuatia ujenzi wa barabara hiyo na wananchi wameridhia
utekelezaji wa mradi huo na kuomba wananchi kutoa mashirikiano wakati wa ujenzi
utakapoanza muda wowote kuanzia mwezi huu .
Amesema ujenzi wa
barabara hiyo pia utahusisha ujenzi wa daraja liliopo katika maeno hayo pamoja
na kuondosha laini za umeme zilizopita eneo la ujenzi wa barabara hiyo.
Nae Mkurugenzi Mkuu
wa kampuni ya ujenzi ya MECCO Abdulkadir Mohammed amesema ujenzi huo utachukuwa
miezi mitano na kumalizika mwezi wa pili mwakani na kukabidhi Serikalini .
Ujenzi huo wa
barabara ya Fuoni Mambosasa hadi Mwera meli sita yenye urefu wa kilo mita 3.4
unaojengwa na kampuni ya kizalendo ya MECCO unafanyika mara baada ya kampuni
hiyo kumalizika daraja la Fuoni Kibonde mzungu na barabara ya Kinuni.



Comments