Serikali yashauriwa kutoisaini sharia na mikataba ya kimataifa ambayo haiendani na Mila na silka za Kitanzania.

Ushauri huo umetolewa na Wakili Abdulkari
Mussa katika semina maalumu iliyowakutanisha watendaji wa taasisi mbali mbali
za kiserikali na binafsi iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari
wanawake Tanzania (TAMWA) juu ya kuzipitia sharia ndogo ndogo zilizopendekezwa
kwa lengo la kupambanha na matendo ya udhalilishaji wa wanawake na watoto
ambazo zitatumika katika shehia zote hapa nhchinhi.
Wakili huyo amesema baadhi ya
mikataba na sharia za kimataifa zinazokuja nchi haziendani na maadili yetu
hivyo hupelekea kuongezeka kwa mmong’onhyoko wa maadili.
Akitolea mfano wa sharia na
mikataba hiyo amesema ni pamoja na sharia na mikataba ya kimataifa
ianayotoa kinga kwa watoto jambo ambalo limewafanya watoto kuwa na uhuru mkubwa
wa kutenda mambo wanayoyataka huku wazazi wao wakikosa uhuru wa kuwaazibu.
"Mimi nakumbuka zamani
ilikuwa ukifanya kosa unacharazwa bakora vizur mpaka unajuta napengine unapigwa
na watu tofauti lakinini saivi wapi mototo anaweza kukushtaki na mzazi ukaingia
hatiani". amesema wakili huyo.
Akichangia katika kipengele kilichowagusa
walimu wa madrasa kilichoeleza kuwa mwalimu kutopokelewa anapotoka
madrasa moja kwenda nyengine hadi nawe na waraka maalum kutoka kituo cha polisi
ili kuonasha kuwa hajawahi kushtumiwa kwa makosa ya uhalifu Afisa fatwa
na utafiti kutoka ofisi ya Mufti Shekh Said Ahmad Mohd amesema ipo haja
kwa serikali kuwasomesha walimum wa madras na kuwapa vyeti ndipo wakafanye kazi
ya kosomesha kama walivyo walimu wa skuli.
"Niwaombe Tamwa muandae
mpango maalum kuiomba Seriakali kuwasomesha walimu wa madras ili na wao wawe na
sifa zenye kutambulika kama walivyo walimu wa skuli hii itasaidiwa kuwapata
walimu walio waaadilifu maana tunaona baadhi ya walimu hawa nao wanashtumiwa
katika kashfa hii". amesema afisa huyo.
Sambamba na hayo amesema kutokuwepo
kwa kinga kwa watoa ushahidi juu ya masuala ya udhalilishaji ndio
sababu iliyopelekea kuongezeka kwa rushwa muhali katika jamii.
Akiwasilisha sherea hizo ndogo
ndogo wakili Walid Mohd Adam amesema lengo la kutungwa kwa kanuni hizo ni
kuweka utaratibu mzuri ambao utasaidia kuzibiti matendo ya udhalilishaji
yasiongezeke katika jamii na sio kama wanavydhani wengine kuwa ni kuungilia
sharia kuu za nchi.
Akihairisha semina hiyo Mratibu wa
TAMWA Pemba Fat hiya Mussa Khamis amewashukuru wote kwa michango yao waliyoitoa
na kusema kuwa marekebisho yatakayofanya kutokana ya michango iliyotolewa
anaamini sharia hizo zitakapo rudi katika shehia na kuanza kutumika zitaleta
mafanikia makubwa katika kupambana na janga la udhalilishaji wa wanawake na
watoto.
Na Othman Ali Juma - Pemba.
Comments