ZFDA jadili muongozo maalum uliotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

WAKALA Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar, (ZFDA) imeanza kujadili muongozo maalum uliotolewa na Jumuiya ya  Afrika Mashariki, wenye lengo la kuinusuru jamii na athari zitakanazo na matumizi ya dawa ambayo hatimae husababisha madhara mbalimbali kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Ofisa kutoka Wakala wa Dawa na Chakula, Mohammed Omar, kwenye Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe katika kikao cha wadau kinachojadili  hatua zinazofaa kuepukana na madhara ya dawa na vifaa tiba.
Amesema lengo la kikao hicho, ni kutengeneza Muongozo ambao utawezesha kufuatilia madhara ya dawa, vifaa tiba, tiba asili, pamoja na chanjo, ili kupata jamii yenye afya bora na kuepukana na maradhi yanayotokana na matumizi ya dawa.
Amesema muongozo huo pia, utaweza kusaidia kuripoti, kuziwakilisha na kizitambua kuchunguza na kufuatilia dawa ambazo zinaleta madhara kwa jamii ,na kuzitafutia hatua za kuzipatia ufumbuzi kwa kutumia njia muafaka bila ya kubadilisha dhamira iliyowekwa na Jumuiya hiyo.
Amefahamisha kuwa kumekuwa na matatizo makubwa ya madhara ya dawa ambazo husababisha kupata maradhi yasiyoambukiza kutokana na jamii kutotumia dawa bila ya kiwango kinachotakiwa.
Alisema wameweka fomu kila kituo cha Afya na hospitali kuzitambua dawa ambazo zinaleta madhara kwa jamii kwa kila mtumiaji ambae atapata madhara baada ya kutumia, ili kupata ufumbuzi na kuisadia muongozo huo kufanyakazi yake, lakini changamoto kubwa iliopo urejeshaji wa fomu hizo ni mdogo.
 Zanzibarleo.

Comments