Wauguzi
Nchini wametakiwa kufanya kazi kwamashirikiano, upendo na uadilifu huku
wakizingatia maadili kwa kuwahudumia wagonjwa kkwenye
wakati unaofaa.
Wametakiwa
kuhakikisha wanatoa huduma zenye usalama na bora kufuatana na mabadiliko ya
sanyasi na teknolojia ili kuboresha utumishi wao kwa wagonjwa na sifa kwa
taifa.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Rashid Hadidi Hamad huko ukumbi
wa baraza la mji chake chake katika maadhimisho ya siku ya wauguzi na wakunga
duniani.
Mkuu
huyo amesema inasikitisha kuona muuguzi anamnyanyasa mgonjwa na kumkejeli jambo
ambalo linavunja heshima na maadili ya kazi yake.
Mapema
afisa uendeshaji tiba Wizara ya afya Pemba Dr Yussuf Hamad Idd amesema wauguzi
wanawajibu wa kujitolea kwa moyo wa huruma na kuwasaidia wengine katika
kuithamini kazi yao.
Katika
risala yao wauguzi hao wamesema licha ya kazi ngumu waliyonayo bado wanakosa
thamani na hukatishwa tamaa kwa kukosa utetezi na kuendelea kuambiwa kwamba
uuguzi ni kazi ya wito.
Comments