Watendaji wa Mahkama watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu.

Image result for MahkamaWAFNYAKAZI wa Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini  Pemba , wametakiwa kufanyakazi kwa kufuata ilani ya Uchaguzi Mkuu wa CCM ya Mwaka 2015/20 katika kusimamia majukumu yao  katika usimamiaji wa haki kwa wananchi  pale wanapokuwa na matatizo  yao kuweza kuyatatua kuyatatua kwa  wakati muafaka.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mdhamini wa Ofisi ya rais Utumishi wa Umma na Utawala bora, Massoud  Ali Muhammed  ,wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi hao  pamoja na kamati ya siasa ya Mkoa wa Kaskazni Pemba  ilofika katika  Ofis ya Mahakam  Mkoa wa Wete, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yao ya kutembelea tasisi za Serikali kuangalia shughuli za  Utendaji wa kazi .

Alisema kuwa Mahkama ni tasisi  muhimu sana kwa serikali kwani nichombo kinacho simamia haki za wananchi wote nchini pale wanapokuwa na matatizo yao na kuweza kuwa tatulia kwa lengo la kuwa patia haki na usawa bila upendeleo .
Alifahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  inaongozwa na ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/ 20 hivyo  ni lazima na viongozi wanaosimamia  tasisi kuitumia ilani kwani ndio imeweka vipengele mbali mbali  vikiwemo vya sheria za nchi  ikiwemo Mahakama ambayo ni mionhoni mwa mihimili mkuu katika serikali kwenye kuongoza nchi.

Hata hivyo aliwambo  Mahakimu hao kuzisimamia kesi zinzofika Mahakamani hapo na kutolewa huku ili kuondosha mrundikano wa kesi kuepusha malalamiko ya wananchi   juu madai yao.

"Mahakimu munayokazi kubwa  ya kuwa elimisha wananchi wanapokuja kusikiliza kesi zao  na kuwapa utaratubu wa kesi zinavyoendeswa ili kuona  haki zao zitapatikana kwa kila anayolalamiko na kuwa imani na mahakama zetu"alifahamisha.

Akizungumzia kesi za udhalilishsji wa Wanawake na watoto na kesi za ubakaji alisema hizi zimekuwa ni nyingi na matukio yanaongezeka  na kuwaomba kutokuzifumbia macho na kutokumuonea mtu muhali kuzitolea hukumu kwa muhusika ili kukomesha matendo hayo.

Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini   Pemba  Mberwa Hamad Mberwa ,alisema lengo la kamati ya sisasa ya Mkoa huo kufanya ziara hiyo kwa Watendaji wa Mahakama ni kutambuana na kujua shughuli za utendaji wa kazi zao ili kuweza kushirikiana pamoja kwenye majukumu yao hasa kipindi cha Uchaguzi Mkuu unaokuja kwani kuna mambo mengi hutokea ya Uvunjifu wa amani  yanayofanywa  na makundi ya watu kuweza kudhibiti hali hiyo  itakapotokea.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ,ambae pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa huo ,alisema kwa sasa ndani ya Mkoa wake  keisi nyingi zimepungua zikiwemo za  Unyanyasaji  wa Wanawake na watoto  ,Ubakaji ,Utumiaji wa madawa ya kulevya kwa kukamatwa na kufikishwa Mahakamani na kuzichukulia hatua kwa  watuhumiwa hao.

Nae Ramadhani Shaib Juma  ,Mjumbe wa kamat hiyo alisema ameridhishwa na majibu ya upande wa mahakama kwa kazi zao wanazozifanya kwa kutoa hukumu kwa mujibu wa sheria zao zinavyowaongoza na kuwaomba wananchi kuzitumia mahakama hizo na kuacha tabia kuzimaliza kesi zao majumbani kwani kufanya hivyo ni kuwatia kasoro mahikumu kuona hawatendei haki wananchi wao.

Akitoa ufafanuzi wa majukumu ya kesi zinazofika mahakamani hapo Naibu Mrajisi wa Mahakama Pemba  Abdilrazak  Abdulkadir ,alisema kwa sasa kesi nyingi zimepatiwa huku tofauti na hapo kipindi cha nyuma kwani watu wengi ilikuwa wanashindwa kutoa ushahid wa kesi za watuhumiwa   mahakamani na kupelekea kuchukua muda mrefu kutolewa hukumu lakini kwa sasa tatizo hilo limepungua kwa kias kikubwa tofauti na  hapo awali.

Comments