Wananchi Wasisitizwa kudai risiti wanapo nunua bidhaa.


Wananchi kisiwani Pemba wametakiwa kulipa kodi kwa wakati nakudai risi pale wanapo nunu bidhaa ili kuiwezesha serekali kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Akizungumza na wananchi wa mji wa chake chake Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB) Makame Khamis mohd amesema ili serekali iweze kutekeleza wajibu wake ipasavyo inampasa kila mwananchi kuweza kulipa kodi na kudai risiti kwa kile watacho kinunua.

Amesema kudai risi kutamuwezesha mteja kuwa na uhakika juu yakile anacho kinunua kuwa kimeweza kuchangia sehemu ya mapato kwa serekali.

Amefahamisha kuwa ili kuondoa uvujaji na ukwepaji wa mapato nilazima kila mmoja anapo uza na kukunua kuhakikisha anakua narisiti na kuiwezesha Mamlaka hiyo kukusanya mapato kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Ameeleza kuwa mafanikio yaharaka hayawezi kupatikana endapo wananchi na wadau wa maendeleo watakwepa kulipa kodi hiyo kila mmoja kwa nafasi yake awajibike ipasavyo na kuleta mabadiliko kwa wananchi wote.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuthamini juhudi zinazo chukuliwa na serekali za kuwaletea maendeleo wakiamini kuwa yote yanatokana na juhudi za kodi zinazo kusanywa Mamlaka ya Mapato Zanzibar ( ZRB ).

Comments