
Akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya maadili ya ndoa kwa wanandoa na wanaotarajiwa kufunga ndoa katika Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar, alisema ndoa nyingi ambazo huzigharimu familia fedha nyingi, hazidumu na kusababisha ongezeko la talaka.
Alisema ndoa hizo zinavunjika katika kipindi kifupi na husababisha familia kubaki katika huzuni.
Aidha alisema subra, uvumilivu na mapenzi ya kweli yanakosekana katika ndoa za sasa tofauti na ndoa za wazee.
Aidha aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kuimarisha ndoa zao kwa maslahi ya vizazi vyao na kuwa walimu kwa jamii.
Naye Katibu wa Mufti, Sheikh Fadhil Suleiman Soraga, alisema serikali kupitia ofisi hiyo imeamua kutoa mafunzo hayo kutokana na ongezeko la talaka na kuwataka wahitimu kuyafanyia kazi mafunzo hayo.
Ofisa Utawala kutoka Ofisi ya Mufti, Sheikh Othman Mohamed Saleh, aliiomba jamii kuchukua fomu na kusisitiza mafunzo yanayotolewa ni bure lengo ni kutoa elimu ya ndoa kwani hivi sasa ndoa nyingi zinavunjika baada ya miezi mitatu.
Kwa upande wao, wahitimu walisema mafunzo waliyopata yatawaongoza namna ya kuwa na mapenzi kwa familia zao, kudumisha ndoa na kutatua migogoro itakayowakabili.
Akisoma risala, Khadija Mussa, aliwataka wanandoa na wanaotarajia kuingia katika ndoa kuhudhuria mafunzo hayo ili kuepusha talaka.
Mhitumu mwengine, Muhoro Haji Ali, kutoka Tumbatu, alisema amejifunza mambo mengi ikiwemo haki za mke, mirathi, talaka, malezi ya mtoto na jinsi ya kutatua migogoro ya ndoa.
Alisema mafunzo hayo sio kwa wanaotaka kufunga ndoa pekee bali hata wale ambao wamo katika ndoa wanatakiwa kupata.
Jumla ya wahitimu 43 walitunukiwa vyeti baada ya kumaliza mafunzo hayo wakiwemo wanawake 26 na wanaume 17.
Zanzibarleo.
Comments