Upepo huo ulozuka kijijini huko haukuwa wa hali ya
kawaida kwani uliwashtua wakaazi wa maeneo hayo na kupelekea kuezuka mapaa
na nyumba moja kuanguka .
Akitoa pole kwa waathirika hao Mratibu wa
kukabiliana na maafa kutoka Ofisi ya Makamo wa pili wa rais Pemba, Khamis
Arazak Khamis, aliwataka waathirika hao kuwa wastahamilivu kutokana na
maafa waliyopata kwani hali hiyo nikutokana na mipango ya Mungu .
Aidha Mratibu huyo aliwataka wanajamii
kuchukua tahadhari katika kujikinga na maafa yanayoweza kutokea kipindi
hiki cha mvua za masika zinazoendelea kunyesha kwa kuondosha miti mikubwa
iliyokaribu na nyumba zao.
"Kwa kweli
wananchi wetu kwanza muwe pole kwa maafa haya kwani mumepata hasara kubwa
lakini tunakuombeni tufuate ushsuri wa watalamu wetu wa mamlaka wa hali ya hewa
kuacha kujenga nyumba karibu na miti mikubwa na sehemu za mabonde yanayokaa
maji".
Nae Sheha wa shehia
ya Stahabu Haji Faki Kombo ,alisema baada ya kutokea maafa hayo jambo la
kwanza alitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya Mkoani ambae ndie mwenye dhamana ya
Wilaya ili kuweza kuchukua hatua kuzifikisha sehemu husika
zinazokabiliana na maafa pamoja na kupeleka majina ya waathirika.
Hata hivyo alisema kuna baadhi ya waathirika nyumba
zao ziliharibika vibaya sana na kulazimika kuwahamisha ndani ya nyumba hizo na
kupatiwa hifadhi ya muda kwa sasa.
Nae Aisha Abdalla Suleiman ,mkaaz wa stahabu
alopatwa na maafa hayo alilazimika kuhama nyumba yake kwani ime ezuka
yote na kwa sasa haikaliki kutokana na hali hiyo.
Kwa upande wake Mtumwa Dadi Shasli miongoni mwa
waathirika wa nyumba yake kuezuka mapaa nae amelazimika kuhama kwa muda.
Hata hivyo aliwashukuru wananchi kwa kushirikiana
kwa pamoja na kuwapa msaada tangu kutokea tukio hilo na kuwaomba viongozi wa
serikali walofika kijijini hapo kuwasaidia .
Comments