Serrekali kuwafikia mafundi walio nje ya mfumo rasmi wa mafunzo.


Image result for mafundi walio nje ya mfumo rasmi wa mafunzo.SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Shilika la kazi Duniani imeanza utaratibu wa kuwatambua mafundi walio nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa kuwapa mafunzo na vyeti vitakavyowasaidia kupata ajira kwa urahisi.

Akizungumza katika kongamano la kuwatambua mafundi hao lililofanyika katika ukumbi wa makonyo Chake Chake Mhandisi kutoka mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Mkubwa Ibrahim Khamis amesema, utaratibu huo utasaidia kuondosha tatizo la ajira kwa vijana.

Amesema kuwa, mafundi waliyo nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, wanakabiliwa na changamoto ya kutotambulika, jambo ambalo husababisha kukosa ajira, kupata malipo kidogo, hivyo vyeti watakavyopewa baada ya mafunzo vitawasaidia kupata kazi na zenye kipato kinacholingana na kazi zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Bakar Ali Suleiman ameeleza kuwa, lengo la kongamano hilo ni utanuzi wa mfumo wa mafunzo ya amali kwenda mbali zaidi mpaka kuwafikia mafundi wasio na vyeti, ili nao waweze kuhakikiwa, kutathminiwa na kutambulika.  

Nae mwakilishi wa Shirika la Kazi Ulimwenguni (ILO) Albert Okali amesema, pamoja na kuwa mafundi hao ndio wengi katika soko la ajira Afrika na ndio wanaochangia nafasi kubwa ya uchumi wa nchi, lakini bado kundi hilo limesahaulika kutokana na kukosa utambulisho rasmi, ambao ndio unaoweza kumpa fursa mbali mbali katika jamii.

Kwa upande wa washiriki wa kongamano hilo walishukuru kupata fursa hiyo ya mafunzo na kupatiwa vyeti na kusema kwamba itawasaidia kutambulika rasmi katika jamii na kupata kazi kwa urahisi.

Kongamano hilo la siku mbili limewashirikisha mafundi mbali mbali waliojifunza nje ya mfumo rasmi wa mafunzo (wasio na vyeti), lilifanyika katika Ukumbi wa Makonyo Chake Chake, kwa lengo la kutambulika katika jamii, ili wapate ajira na kuondokana na maisha duni.

Comments