
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi (Gavu), alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Alisema kati ya fedha hizo, shilingi shilingi 9.72 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kazi za kawaida na shilingi 2 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Alisema kuna ongezeko la shilingi milioni 232.6 sawa na asilimia tano ikilinganishwa na bajeti inayotekelezwa sasa.
Alisema kwa upande wa mradi wa maendeleo bajeti imeongezeka kutoka shilingi bilioni 1 hadi shilingi bilioni 2 sawa na asilimia 100 ya ongezeko.
Alisema kwa mwaka ujao wa fedha, ofisi ya Rais, imejipanga kutekeleza vipaumbele ikiwemo kuratibu shughuli na kusimamia huduma za Rais, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa shughuli za wizara, idara na taasisi za serikali pamoja na maamuzi ya serikali.
Alisema kipaumbele chengine ni kuratibu ushiriki wa watendaji wa serikali katika vikao vya mtangamano wa jumuiya za kikanda na kusimamia majukumu ya kikatiba na kisheria ya Baraza la Mapinduzi.
Akizungumzia programu ya kuratibu ushirikiano wa kikanda, mashirika ya kimataifa na wazanzibari wanaoishi nje, alisema lengo la program hiyo ni kuimarisha na kuendeleza ushiriki wa Zanzibar katika mikutano ya jumuiya za kikanda, kimataifa na kuwashirikisha ipasavyo wazanzibari wanaoishi nje katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Alisema matokeo ya utekelezaji wa programu hiyo ni kuendelea kufaidika kwa wazanzibari na fursa za kiuchumi na kijamii zinazotokana na jumuiya za kikanda, kimataifa na wazanzibari wanaoishi nje ya nchi.
Aidha alisema katika kufikia malengo ya programu hiyo, shughuli za utekelezaji zimepangwa ikiwemo kusimamia shughuli za kila idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi, kujenga uelewa kwa jamii juu ya sera ya diaspora na utekelezaji wake, kushiriki katika mikutano ya ndani na kimataifa inayohusiana na diaspora.
Zanzibarleo.
Comments