
Hii
ni mara ya Pili kwa daraja hilo kujaamaji kama ilivo tokea mwaka 2017 katika
mvua zamasika.
Barabara
hii ni njia kuu inayotumiwa na wananchi waliowengi kisiwani Pemba katika
kufuata huduma kutoka mkoa mmoja kwenda mwengine.
Wakizungumza
kwa maskitiko wananchi walio kwama katika eneo la Daraja la chamanangwe Wilaya
ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba wamesema ipohaja kwa Serekali ya Mapinduzi
Zanzibar kulishulikia daraja hilo kwani mvua zinapokua kubwa hujaamaji na
kushindwa kuendelea na safari zao zakujitafutia maisha.
Aidha
wameitaka Wizara ya ujenzi na Usafirishaji kuwatatulia kesro za daraja hilo
kwani ndio njia pekee inayo warahisishia kufika makazini kwa muda muafaka.
Kwamujibu
wa vyanzo vyetu vya habari hali hii pia imejitokeza katika daraja la Piki
kadhalika katika maendeo ya Vitongoji.
Comments