‘Malimbikizo nauli za walimu kulipwa’.

SERIKALI imesema kuwa italipa malimbikizo ya fedha za nauli kwa walimu ambao hawajapewa fedha hizo.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Kijitoupele, Ali Suleiman Ali.
Mwakilishi huyo katika swali lake hilo alitaka serikali kupitia wizara ya elimu na tawala za mikoa kukaa pamoja kuhakikisha wanawapa nauli hiyo ili kuweza kufika kazini kwa wakati.
Alisema kwa walimu wa skuli za msingi suala hilo la nauli linasimamiwa na wizara yake na wale walimu ambao bado hawajapatiwa nauli hiyo watapatiwa.
Akijibu swali la msingi, lililoulizwa na mwakilishi huyo, Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Simai Muhamed Said, alisema tokea kuanza kazi kwa mfumo wa ugatuzi wenye dhamana ya malipo ya nauli kwa walimu wa skuli za msingi ni halmashauri, manispaa, mabaraza ya miji.
Awali Mwakilishi huyo alisema kuna malalamiko ya kukosa nauli za usafiri kwa walimu wa skuli za msingi wilaya ya kati kwa muda wa miezi minne na kusababisha usumbufu kwa walimu hao.
Zanzibarleo.

Comments