Kamati ya siasa Kaskazini Pemba Yafurahishwa na Utendaji wa CCM.


Related image
KAMATI  ya siasa ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, imesema imefurahishwa na utekelezaji wa shughuli za wizara ya kilimo katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi  CCM ya mwaka 2015-2020 katika kuwapatia huduma wananchi wake.

 Mwenyekiti wa Kamati ya siasa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mberwa Hamad Mberwa ameseyasema hayo katika kikao cha majumuisho ya ziara ya kukagua maeneo ya Wizara ya Kilimo kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi   (CCM ).

Mberwa amesema, kupitia Chama cha Mapinduzi kamati yao itaendelea kutoa ushirikiano  na Wizara ya kilimo kwa kufuatilia utekelezaji katika kufikia malengo ya Ilani pamoja na kupambana na wanaofanya uharibifu wa rasilimali za nchi kwa faida ya taifa.

Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo ,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Pemba, Sihaba Haji Vuai, amesema kwa kiasi kikubwa imekuwa ikijitahidi kutekeleza majumu yake kwa kwa ufanisi lakini wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya watendaji wa serikali.

Mapema akitoa maelezo kwa kamati ya siasa, juu ya  uoteshaji wa miche ya minazi huko Chamanangwe, Afisa Mkuu Idara ya Misitu na Mali asili zisizorejesheka, Said Juma Ali, amesema wanategemea kufanikiwa katika utekelezaji wa Programu ya kurejesha uoto wa asili ya minazi kwa asilimia 98.

Kwa upande wao wananchi waliobahatika kukaguliwa, Miradi yao wamesema wamefajika sana kutokana uamuzi wa Serikali kufanya ziara za kuwaona juhudi zao pamoja na kuwasaidia kila hali itakapo ruhusu.

Comments