Dr. Shein asisitiza elimu itolewe kwa wananchi waweze kuzijua sheria za nchi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesistiza haja kwa Wizara ya Katiba na Sheria kuandaa taratibu maalum za kuwaelimisha wananchi kuhusiana na sheria mbali mbali zilizopo nchini. 

Dk. Shein amesema hayo Ikulu ndogo Kibweni mini Zanzibar, alipokutana na Uongozi wa Wizara Katiba na Sheria, wakati ilipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai 2018 hadi mwezi Machi 2019.

Alisema utowaji wa elimu hiyo utawasaidia wananchi kufahamu kwa kina uwepo wa sheria mbali mbali na hivyo kuondokana na mkanganyiko katika masuala mbali mbali yahususuyo sheria. 

Dk. Shein alieleza kufurahishwa kwake na kazi nzuri iliyofanywa na Wizara hiyo katika utekelezaji wake wa majukumu, ikiwa pamoja na kukabiliana na changamoto mbali mbali za kiutendaji.

Wakati huo huo,    Waziri wa Wizara ya kazi, Uwezeshaji, Wazee, wanawake na watoto, Moudline Castico  aliwasilisha utekelzaji wa mpango kazi wa Wizara hiyo alisema katika kipindi hicho Wizara iliratibu na kusimamia utekelezaji mpango wa pensheni jamii kwa wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea, ambapo jumla ya wazee 27,783 wanaopokea pensheni hiyo Unguja na Pemba hadi kufikia mwezi Machi, 2019.

Alisema imeratibu upatikanaji wa ajira kwa wananchi 1,555 Unguja na Pemba, kupitia sekta binafsi ikiwemo hoteli , skuli binafsi na taasisi nyengine, sambamba na kuratibu ajira za nje ya nchi kwa  vijana 1,033.

Aidha, Waziri Castico alibainisha kuwa Wizara hiyo imefanya ukaguzi maalum kwa taasisi 376 kuangalia utekelezaji wa agizo la kima cha chini cha mishahara.



Comments