Bright Security yapewa ushauri.


Kampuni Ya Ulinzi ya  Bright Security Company Limited ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba imetakiwa kuwa karibu na Jeshi la Polisi Mkoani humo ili kuweza kupata ushauri na maelekezo kwa lengo la kufanikisha Utendaji wa majukumu ya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Ushauri huo umetolewa na SSP Hamad Mbarouk Rashid  ,ambae ni Mratibu Mwandamizi wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba , hapo Ukumbi wa Jamuhuri holi Wete wakati alipokiwa akizindua rasmi Campuni  hiyo.

Alisema kufunguliwa kwa Campuni hiyo   ndani ya Mkoa huo itaweza kusaidia harakati za ulinzi  katika  Ofisi za Serikali na tasisi za watu binafsi kwani ni muhimu sana katika jamii  itakuunguza matendo ya wizi na uhalifu .

Aidha alisema kuwa vijana hao wanatakiwa kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea pamoja na kuwa na Uzalendo wa kuipenda nchi yao kwa kutoa ulinzi hata kwenye shughuli za kitaifa.

"Mm niwapongeze vijana haoambao kwa kukubali kujitolea kunda Campuni na Wazee walotoa wazo hilo  wamefanya jambo zuri la kupigiwa mfano sasa fanyeni kazi vijana " alisema.

Mratibu huyo wa polisinaliwaomba vijana hao kuwa na uwadilifu kwenye kazi na kujiepusha na matendo ya rushwa kwani yatashusha hadhi na heshima kwenye Campuni yao na kukosa uwaminifu.

Said Omar Said ,ambae ni miongoni wa vijana hao wa Campuni ua Ulinzi ya Bright Security ,alisema  watatenda haki kwenye kazi zao na kujiepusha na matendo ya rushwa ambayo yatashusha nidhamu ya ulinzi.

Hata hivyo aliwaomba wafanya biashara  na tasisi za serikali kuwatumilia kwenye kazi za Ulinzi kwani wengi wao wamepata kozi  wamepata mafunzo kutoka Jeshi la kujenga Uchumi JKU   ,JKT na Mafunzo ya mgambo  na kuwafanya kujua sheria za ulinzi  na mambo mengine.

Kwa upande wake Asya Hamad Omar ,alisema kupitia Campuni hiyo Mkoa wa kaskazini Pemba umejikomboa kwani ndio mara ya kwanza kufanyika jambo hilo.

Akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi na wageni walikwa Mzee wa kamati hiyo  Muhammed Said Muhammed ,wamelishukuru jeshi la polisi kwa kukubaliana ombi lao la kuundwa kwa Campuny hiyo na kuwataka kuilea na kuwapa maelekezo ya kiulinzi pamoja na kuwapatia baadhi ya vifaa  ambavyo watavihitaji kwenye kazi zao.

Hata hivyo aliwaomba wananchi wa Wete na Mkoa mzima wa Kaskazini kuiyunga mkono Campuny hiyo ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaid.

Comments