Benki yadamu Salam Zanzibar yavuka malengo yavuna uniti 2,100.

JUMLA ya uniti 2,100 za damu zimekusanywa katika bonanza la uchangiaji damu kwa ajili ya kuweka akiba ya mwezi mtukufu wa ramadhan.
Meneja wa uhusiano wa benki ya damu salama Zanzibar, Bakari Hamadi Magarawa, aliyasema hayo wakati akitoa majumuisho ya zoezi la uchangiaji damu kwa hiyari huko ofisini kwake.
Magarawa alisema lengo la benki hiyo ilikuwa kupata uniti 1,700, lakini wamevuka lengo kwa kukusanya uniti 2,100.
Alisema akiba hiyo itasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wakiwemo akinamama wajawazito na wenye mahitaji mengine wakiwemo wale wanaopata ajali.
Meneja huyo ambaye pia ni katibu wa jumuiya ya uchangiaji damu Zanzibar, alisema tangu kuanza bonaza hilo limeweza kuzaa matunda mazuri ya upatikanaji wa uhakika wa damu katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhan.
“Bonanza hili lilianzia maeneo ya Fumba kwa Zanzibar na kuanza zoezi hilo katika wilaya zote za Unguja na Pemba”, alisema.
Aidha alisema upatikanaji kwa kiwango hicho cha damu wataweza kusaidia hospitali zote za Unguja na Pemba.
Alisema kuwa kufanikiwa kwa zoezi hilo ni moja ya juhudi zilizofanywa na kitengo cha damu salama kwa mashirikiano na wadau mbali mbali wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa.
Alisema kuanzia mwaka jana tangu kubuniwa kwa bonanza maalum la uchangiaji damu kwa hiyari kumeweza kupatikana damu ya kutosha katika kipindi cha mfungo.
Alisema wilaya zote wameweza kuchangia damu kwa mujibu wa mpango  mkakati wao walivyojiwekea.
Alisema kipindi cha ramadhan kunakuwa na ajali nyingi kipindi cha usiku kila mmoja anakimbilia kufutari na huwa wanapokea ajali za mara kwa mara na wengine wanakufa kutokana na chanagamoto ya upatikanaji wa damu.
Zanzibarleo.

Comments