Jeshi
la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limesema linamtafuta Nd. Khamis Ali Diri
anaetuhumiwa kumpa ujauzito mwananfunzi wa darasa la 6 Skuli ya Msingi Kengeja.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa huwo Hassan Nassir Ali amesema mtuhumiwa huyo baada ya
kufanya tendo hilo na kukimbilia Kisiwani Unguja ambapo Jeshi la Polisi
linaendelea na Msako wa kumtafuta ili kumpeleka katika vyombo vya sheria.
Kamanda
Nassir amesema tayari wamesha wasiliana na Polisi wa Mkoa wa Mjini Maghribi ili
kuhakikisha mtuhumiwa huyo aliempa ujauzito Shemegi yake Alie muolea dadaake
baba mmoja mama mmoja anakamatwa maramoja.
Wakati
huo huo Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba amesema wanaendelea na uchunguzi
wa kupewa ujazito mwanamke mwenye umri wa miaka 24 ambae ni bubu na mlemavu wa
akili huko kaani shehia ya kengeja.
Amefahamisha
kuwa majalada ya kesi hizo yanaendelea kushughulikiwa kwa taratibu za Kipolisi.
Comments