Watendaji wa wizara ya kilimo watakiwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.


Image result for manga mjengo mwajiri
Waziri wa Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri, amewataka watendaji wa wizara yake wanaoshughulika na uoteshaji na ugawaji wa miche kuacha kutekeleza majukumu kwa kutumia mazoea na badala yake kusimamia na kufatilia uoteshwaji wa miche inayotolewa kufikia lengo la serikali.

Mh. Mmanga ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati alipofanya ziara fupi yakutembelea nasari za kuotesha  miche ya mikarafuu huko mkata maini na chanjaani wilaya ya chake chake.

Amesema, iwapo maafisa watasimamia vyema katika malezi ya miche itakayotolewa itasaidia miche kustawi zaidi kwa kuisaidia serikali kuweza kutimiza malengo yake ya kunyanyua wananchi.

Kwa upande wao, wafanyakazi wa nasari za miche ya mikarafuu wameahidi kusimamia vyema taratibu zinazohitajika ili kukamilisha malengo yalio kusudiwa.

Aidha wameiomba serikali kupitia wizara husika kuwatatulia changamoto ya upatikanaji wa maji na kuongezewa wafanyakazi , katika kuimarisha ongezeko la miche ambayo ndio kilio cha wananchi.

Comments