
Samaki mkubwa mwenye urefu wa zaidi ya mita kumi na
tano, upana mita saba anaejulikana kwa jina maarufu chongowe
ameonekana katika bahari ya kinowe , wilaya ya micheweni, mkoa wa
kaskazini pemba ambapo wananchi wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya samaki
huyo ili kunusuru kutokea madhara.
Akizungumza
na wananchi huko katika bandari ya kinowe wilaya ya micheweni kaimu afisa mkuu
wa idara ya maendeleo ya uvuvi Hidaya Khamis Hamad, amewaasa wananchi
kutomtumia samaki huyo kwa matumizi ya kula, ili kunusuru afya zao.
Kwa
upande wake, afisa uvuvi pemba , aAli Rashid Hamad, amesema idara ya maendeleo
ya uvuvi kwa kushirikiana na taasisi nyengine watafanya
uchunguzi ili waweze kutambua aina ya
samaki kwa faida ya jamii na taifa kwa ujumla.
Nae sheha
wa shehia ya kinowe Juma Adi Haji amesisitiza juu ya matumizi sahihi
ya mafuta ya samaki huyo ,ili waweze kuwa salama.
Kwa
upande wao wananchi waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kuchukua mafuta
akiwemo Asaa Hamad Ali amesema watatumia mafuta hayo kwa ajili ya
tiba na si vyenginevyo kwa kufuata maelekezo na ushauri wa serikali.
Comments