WAFANYAKAZi wa Kituo cha Mkono kwa Mkono wa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoai Kisiwani Pemba wametakiwa kuelimisha jamii kuhusiana na vitendo vya udhalilishaji vinavyoendelea siku hadi siku.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mdhamini wa Wizara ya afya Pemba Shadya Shaaban Seif ,katika Uzinduzi wa Kituo cha Mkono kwa Mkoani hapo hospitali ya Abdalla Mzee ,alisema nivyema kwa wafanyakazi wa kituo hicho kuwa na mashirikiano ya pamoja kwa kutoa elimu kwani vitendo Vya Udhalilishaji vinafanywa na jamii husika.
Alifahamisha kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatilia mkazo kupiga vita mambo ya Udhalilishaji ili kujenga misingi mizuri kwa mustakbali wa maisha ya wananchi na taifa kwa ujumla.
"Kufunguliwa kituo hiki hospitalini hapa wananchi wa Mkoani kitasaidia kupunguza matendo ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia kwani ndio njia moja ya kuchukuliwa hatua watu wanaofanya uwovu huo".alisema .
Afisa Mwandamizi ,Ulinzi wa Watoto wa shirika la kuhudumia watoto the save the children kwa upande wa Zanzibar ,Shaib Abdalla Muhammed, alisema vito vya mkono kwa mkono ni muhimu katika kushughulikia kesi za watoto waliofanyiwa udhalilishaji .
Aidha alisema matendo ya udhalilishaji yamekuwa ya kifumbiwa macho na kuchangia kuongezeka kwa kuoneana haya na rushwa muhali ya kuwachukulia hatua kwenye vyombo husika.
"Wafanyakazi mloaminiwa kufanyakazi kazi kuweni wadilifu na musimamie haki kwa mtu atakae pata kesi za udhalilishaji kwani rushwa muhali na kuoneana aibu imetawala ".alisema.
Nae Afisa Uwendeshaji tiba kutoka Wizara afya Pemba ,Dr Yussuf Hamad Iddi, ameliomba shirika la save the Chidren kuendelea kuanzisha vituo maeneo mengine kikiwemocha hospitali ya Vitongoji Kotej ili wananchi wamaeneo hayo waweze kupata huduma kiurahis na kuwafanya wahanga hao wasiendelee kuathirikia zaid.
Akitoa shukurani kwa shirika hilo Mganga Mkuu wa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani ,Haji Mwita Haji, alisema kwa sasa shughuli zitaendelea kupatikana kwa uhakika baada ya kupatiwa vifaa vya kutendea kazi kwa ufanisi zaidi.
Kufunguliwa kwa kituo cha Mkono kwa Mkono hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani itakuwa kimbilio la wahanga wanakutwana matendo ya udhalilishaji.
Comments