
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Riziki Pembe Juma ametangaza matokeo ya mitihani ya darasa la nne, darasa la sita na kidatu cha pili.
Akitangaza matokeo ya mtihani wa Darasa la sita amesema ufaulu unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 33,519 kati ya 34,822 sawa na asilimia 96.3 waliofanya mtihani huu wamefaulu wakiwemo wanawake 18,160 sawa na asilimia 52.2 na wanaume 15,359 sawa na asilimia 44.1, wanafunzi 1,303 sawa na asilimia 3.7 hawakufaulu. Ufaulu huu umeongezeka kwa asilimia 0.1 ikilinganishwa na ufaulu wa asilimia 96.2 ya mwaka 2017.
Matokeo ya jumla ya Mtihani wa Kidato cha Pili mwaka 2018 yanaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,907 sawa na asilimia 73.25 wakiwemo wanawake 13,986 sawa na asilimia 42.85 na wanaume 9,921 sawa na asilimia 30.40 kati ya watahiniwa wote 32,636 waliofanya mtihani huu wamefaulu. Wanafunzi 8,719 sawa na asilimia 26.72 hawakufaulu. Ufaulu huu wa mwaka 2018 umeongezeka kwa asilimia 0.97 ikilinganishwa na ufaulu wa asilimia 72.28 wa watahiniwa wa Kidato cha Pili waliomaliza elimu ya msingi wakiwa Darasa la Sita mwaka 2017.
Skuli ya FEZA inaongoza kwa Mtihani wa Darasa la Nne, Trifonia Academy inaongoza kwa mtihani wa Darasa la Sita na Skuli ya Sekondari ya Lumumba inaongoza kwa mtihani wa Kidato cha Pili.
Comments