Waziri wa afya wa Zanzibar Mh, Hamad Rashid Muhammed, amewaomba madaktar wa hospitali ya Chake chake kushirikiana na madaktar kutoka nchini Uhispania wanaoendelea kutoa matibabu kwa akina mama pamoja na akina baba ambao wanasumbuliwa na matatizo mbali mbali hasa mishipa.
Amesema kuwa madakari hao wameamua kufika kisiwani Pemba kwani wameona wananchi hao wanashindwa kujitibu na kuendelea kuathirika siku hadi siku na kuwataka kuitumia fursa hiyo ili kupata matibababu bure.
Mh Hamad amesema haitokuwa jambo la busara kwa madatari hao kuondoka hospitalini haopo bila ya madaktari wazalendo kupata ujuzi ili waweze kuendeleza huduma za matibabu pale watakapo ondoka kisiwani Pemba.
Nae Naibu wa Waziri wa afya wa Zanzibar Mh,Harusi Said Suleiman ,amewapongeza madaktar bingwa kwa kuweza kutoa matibabu kwa wananchi wa Kisiwa cha Pemba kwani wameweza kuokoa uhai kwa wagonjwa hao.
Aidha aliwataka wagonjwa wote ambao wamepatiwa matibabu na madaktari hao kuendelea kutumia maelekezo walipewa ili kuepeka kutokea athari hapo baadae.
Kwa upande wake wake kiongozi wa madaktari hao kutoka nchini Uhispania Rosa Barrachina ,amesema kuwa timu ya madakari kumi imefika hospitali ya Chake chake kwa lengo la kutoa huduma kutona na hali duni za maisha yao kwa kuto mudu gharama za kwenda nchini huko kutibiwa.
Amesema magonjwa wanayotoa matibabu ni mayoma kwa akina mama ,Uvimbe kwenye mizizi ya mishipa ya Uzazi na magonjwa mengine yakinamama na kwa akina baba ni Mishipa ya ngiri na hania.
Comments