Watendaji wa Wizara ya Afya Pemba watakiwa kuwa na mashirikiano kazini.

Image result for hamad rashid
Wafanyakazi wa Wizara ya afya kisiwani Pemba wametakiwa kuwa na mashirikiano  mazuri kwenye utendaji wa kazi pamoja na kutumia lugha nzuri kwa watu wanao wahudumia.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashidi Muhammed ,wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa wizara hiyo na watendaji wa hospitali tano za Pemba huko  ukumbi wa maabra ya Jamii Wawi Chake chake Pemba.

Alisema kila siku zikienda mbele ushirikiano huo unapungua na kuwataka viongozi kufatilia matatizo kwa wafanyakazi wao ili hali hiyo irejee kama ilivyokuwa mwanzo.

Hata hivyo aliwaomba wafanyakazi kutumia maadili yakazi vizuri na kuacha kutoa siri za ofisi kwani kufanya hivyo ni makosa kisheria na kumuagiza ofisa mdhamini kuwafatilia wafanyakazi watakaobanikia kufanya hivyo ili kuchukuliwa hatua.

Akizungumzia usafi katika hospitali amesema bado hali hairidhishi ingawa viongozi wanajitahidi kusimamia lakini  juhudi zaidi zina jitajika.

Nae Naibu wazir wa Wizara ya afya Zanzibar Harusi Said Suleimani ,alisema hafurahishwi kuona wafanyakazi wake wamekosa ushirikiano  kwenye sehemu za kazi jambo ambalo  linapunguza maelewano  na uwajibikaji kazini.

Hata hivyo alisema kuwa wafanyakazi wa Wizara ya afya wote ni watoto wa nyumba moja hivyo wanatakiwa kuwa na umoja na mshikamano  ndio kitu pekee kinacho ongeza upendo  na ufanisi zaid.

Kwa upande wake afisa Mdhamin wa Wizara ya afya Pemba Shadya Shaabani Seif ,amewaomba wafanyakazi wake kubadilika na kuacha kufanyakazi kimazoe na kuwatumkia wananchi ili kupata huduma zilobora .

Comments