Walio teuliwa na Dr. Shein waapishwa Ikulu Zanzibar.

Image may contain: 2 people, people standing and beard
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Hamida Mussa Khamis ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja, Khalid Abdalla Omar anaekuwa Naibu Katibu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.
Mwengine aliyeapishwa hivi leo ni Omar Said Ameir anaekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.
Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih.
Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na Washauri wa Rais wa Zanzibar, viongozi wengine wa Serikali pamoja na wanafamilia.
Mapema wafanyakazi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ofisi ya Faragha ya Rais walimtakia kheri ya siku ya kuzaliwa Rais Dk. Shein ambaye amezaliwa Machi 13, 1948.
Image may contain: 2 people, people standing and beard
Image may contain: 5 people, people standing

Comments