
WAKUNGA wa jadi wametakiwa kuhamasika kuwapeleka kinamama wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya, ili kupunguza vifo vya kinamama na mtoto.
Ofisa Elimu ya Afya Wilaya ya Magharib ‘A’ Fatma Ali Khatib, aliyasema hayo wakati akizungumza na wakunga wa jadi wakijadili changamoto za mama wajawazito wakati wanapozalishwa majumbani, ili kuhamasika kuwapeleka hospitali.
kikao hicho kilichowakutanisha wahudumu wa afya wa kujitolea ngazi ya jamii kilichofanyika skuli ya Langoni.
Alisema kumekuwa na baadhi ya wakunga bado wamekuwa wakaidi kuwazalisha kinamama wajawazito majumbani jambo ambalo linasababisha kutokea kwa wimbi la vifo vya kina mama na watoto.
Alisema wameanza kutoa elimu kwa jamii ili kusaidia kupata idadi kubwa ya wanaojifungulia katika vituo vya afya na vifo vya akinamama na watoto wachanga vitapungua.
Akizungumzia sula la changamoto liliopo katika vituo vya afya juu ya ukosefu wa vifaa vya kinamama wajawazito ikiwemo Ultrasound, kipimo cha mkojo , presha na damu .
alisema Wilaya yake ipo mbioni kutafuta huduma hizo ikiwa pamoja na kukunua japo moja ili kusogeza huduma hizo kwa mama wajawazito na kupunguza msongomano katika hospitali ya Mnazimmoja.
Alisema pamoja na taarifa kuwa zinakosekana hivyo Wilaya ya Halmashauri imeona kuweka wahudumu wa afya wa kujitolea ngazi ya jamii, ili kusaidia upatikanaji wa taarifa kwa wakati na kuzipatia ufumbuzi ili kuweza kunyanyua afya bora kwa mama, baba na mtoto.
Zanzibar.
Comments