
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Dkt Idrisa Muslim Hija amesema uanzishwaji wa ripoti ya awali ya upitiaji na uwendelezaji wa mtaala wa elimu ya Maandalizi na Msingi italeta mwelekeo mzuri na kuondosha malalamiko ya wananchi.
Akifungua mkutano wa uwasilishwaji wa ripoti ya awali katika ukumbi wa Takwimu Mazizini amesema baadhi ya Viongozi na wananchi wamekuwa wakilalamika juu ya mitaaala ya elimu ya ngazi za Maandalizi na Msingi kwa wanafunzi kusomeshwa masomo mengi hali inayowapelekea kubeba mzigo mkubwa wa Mabuku.
Amesema mapitio ya ripoti hiyo yanafanyika kufuatia mtaala huo kuwa umetumika kwa muda mrefu hivyo marekebisho yake yatasaidia mitaala hiyo kuendana na wakati uliopo.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Zanzibar Bw. Sleiman Yahya amesema kutokana na shughuli za ugatuzi Skuli za Maandalizi na Msingi zimepewa mamlaka halmashauri kuzisimamia hivyo amewataka watendaji wa halmashauri hizo kutoa mashirikiano kwa kutoa maoni yao juu ya ripoti hiyo ili kuiletea ufanisi zaidi.
Amesema kukamilika kwa ripoti hiyo kutafuatiwa na ufuatiliaji pamoja na majaribio juu ya utekelezaji wake .
Nao washiriki wa mkutano huo wamesema marekebisho ya mtaala huo utasaidia wanafunzi kupata elimu bora na mitaala etaendanana ushindani wa kielimu kwa wanafunzi.



Comments