
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed
Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibr kama ifuatavyo:-
1.
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAAA NA IDARA
MAALUM ZA SMZ.
i. Mkuu wa Wilaya ya Kati -Bibi
Hamida Mussa Khamis.
ii. Naibu katibu Mkuu katika
ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ
anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – Bwana Khalid Abdalla
Omar.
iii. Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kusini, Pemba – Bwana Abdulla Rashid Ali.
iv. Katibu Tawala Wilaya ya
Chake Chake – Bwana Omar Juma Ali.
1.
OFISI YA RAIS, UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA.
i. Mkurugenzi wa Mipango, Sera na
Utafiti katika Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Bwana Yussuf
Mohammed Ali.
ii. Mkurugenzi wa Uendeshaji na
Utumishi katika Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Bwana Bakari
Khamis Muhidini.
1.
WIZRA YA KATIBA NA SHERIA.
i. Mkurugenzi wa Idara ya
Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Katiba na Sheria- Bibi Daima Mohamed
Mkalimoto.
ii. Mkurugenzi wa Uendeshaji na
Utumishi katika Wizara ya Katiba na Sheria – Bwana Juma Ali Simai.
1.
WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI.
i. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Utafiti wa masuala ya Uvuvi na mazao ya baharini katika Wizara ya Kilimo,
Maliasili, Mifugo na Uvuvi- Dkt. Nariman Saleh Jidawi.
ii. Mkurugenzi wa Idara ya
Uhakika wa Chakula na Lishe katika Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi-
Bwana Hamadi Masoud Ali.
1.
WIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE.
i. Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(Maelezo) – Dr. Juma Mohammed Salum.
ii. Katibu Mtendaji wa Tume ya
Utagazazi ya Zanzibar- Bwana Omar Said Ameir.
1.
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA , MAJI NA NISHATI. Mkurugenzi wa
Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati –
Bwana Yussuf Amour Ali.
Comments