Viongozi wa serekali za mitaa wametakiwa kuzingatia maslahi ya umma ili kutekeleza haki kwa wanao waongoza.
Akizungumza na wasaidia wa sheha wa shehia ya uweleni huko katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkoani afisa kutoka Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Haji Juma Chapa amesema viongozi hao wamepewa dhima kubwa kuweza kuwaongoza wananchi hivyo sivyema kutenda upendeleo kwa wengine na badala yakwe watende sawa kwa wote.
Amesema ili kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo wanatakiwa kujiepusha na migongano ya kimaslah ambayo itawasababishia kutoa maamuzi kwa upendeleo.
“ukiwa kiongozi unatakiwa kuwa muadilifu na hupaswi kutoa upendeleo wakati unapo toa maamuzi yako”.
Nae Suhaila Mohd Iddi afita kutoka Tume ya maadili kwa Umma amewaomba viongozi hao kufuata sheria katika maamuzi yao ili wananchi waendelee kuwaamini nakutoa mashirikiano kikamilifu.
“Endapo kiongozi atajihusisha na matendo ambayo hayana maadili badi kutaleta athari za kutopiga hatua za kimaendeleo”.
Aidha amewasili kutojiingiza katika matendo yatakayo waingiza katika uvunjifu wa maslah ya Umma ili maendeleo yaharaka yaweze kufikiwa.
Nao wasaidizi hao wa sheha shehia ya Uweleni wameahidi kuyafanyia kazi yale yote waliopatiwa ili wawe watendaji wazuri kwa serekali na jamii kwa ujumla.
Comments