CUF kuwapeleka mahakamni ACT-Wazalendo.

CHAMA cha CUF kimefungua kesi Mahakama Kuu iliyopo Vuga mjini Zanzibar, dhidi ya watu waliohusika kubadili rangi za ofisi zake, ambazo zimetiwa rangi inayodaiwa kuwa ni ya chama cha ACT- Wazalendo na wale waliochoma moto bendera za chama hicho.
Akizugumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katibu mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman Khalifa alisema kuwa kesi hiyo imefunguliwa baada ya kukusanya ushahidi wa matukio hayo.
Halifa alisema kuwa ushahidi uliopatikana na majina ya wanaodaiwa kuhusika kuchoma bendera ya CUF, kubadili rangi za ofisi ya chama hicho na kupaka rangi na nembo za chama cha ACT-Wazalendo.
Aidha alisema kuwa walikubaliana wakusanye ushahidi kwa waliofanya matukio hayo na majina ya waliofuta rangi za chama hicho na waliochoma moto bendera za chama.
Alisema wakitaka chama cha ACT Wazalendo kufungua matawi mapya na kama wanadhani kuwa ni busara na kufanya ofisi za CUF kuwa ni zao kwa kisingizo cha wananchi.
Alisema yapo majengo ya ofisi za chama hicho yamenunuliwa kwa pesa za chama ambapo baadhi yao zimetumika zaidi ya shilingi milioni 150, miaka mingi iliyopita hivyo hawawezi ofisi hizo zirithiwe na ACT – Wazalendo.
“Tumefungua kesi katika mahakama Kuu ya Vuga visiwani Zanzibar na sasa sheria itachukua mkondo wake”, alisema khalifa.
Alisema msemo wa shusha tanga pandisha tanga wa chama cha ACT- Wazalendo utaishia kwa kukaa matanga hasa kutokana na tabia ya kudhani mtu ni chama.
Alifafanua kuwa, wabunge wajue kuwa waliingia katika bunge kwa tiketi ya chama cha CUF, hivyo wasije wakadhania kuwa aliowapeleka bungeni ni Maalim Seif, wao wameingia bungeni kwa tiketi ya Chama cha wananchi CUF.
Alibainisha kuwa wao hawatakubali kuona watu wanatumia pesa na rasilimali za CUF kuiimarisha chama cha ACT-Wazalendo kuna mawili, wajiandae kurudi au wasubiri mengine.
Hata hivyo, kubadilishwa kwa rangi za Chama pamoja na kupachuliwa kwa bendera za chama cha CUF, kimetokea baada ya Prof. Ibrahim Haruna Lipumba kushinda kesi katika mahakama Kuu ya Tanzania, kuwa Mwenyekiti halali wa Chama cha CUF, hali ambayo iliyompelekea Maalim Seif Sharif Hamad kuamia chama cha ACT wazalendo.
Zanzibarleo.

Comments