Waziri atoa sababu zinazochelewesha wananchi kufungiwa mita za umeme Zanzibar.

Naibu Waziri wa Ardhi Maji na Nishati Zanzibar  Juma Makungu Juma amefafanua sababu zinazochelewesha kufungiwa mita za umeme kwa wananchi wa Zanzibar.
Ufafanuzi huo ameutoa Jana katika kikao cha baraza la wawakilishi alipokuwa akijibu swali la Ali Suleiman Ali mwakilishi wa jimbo la Kijitoupele  (CCM),Unguja alietaka kujua tatizo linalosababisha ucheleweshaji wa upatikanaji wa mita za umeme kwa wananchi visiwani zanzibar
Naibu Waziri akitoa ufafanuzi huo alisema miongoni mwa sababu zinazopelekea kuchelewesha ufungaji wa mita za umeme kwa wananchi ni kutokana na kutokuwepo kwa vifaa vya kutosha ikiwemo mita zenyewe.
“sababu kubwa ni kuchelewa kufika kwa vifaa ikiwemo mita pamoja na kutosha kwa vifaa vingi kwa umeme” alifafanua Naibu Waziri.
Hata hivyo alisema kwa sasa wanampango wa kuanza kuwafungia wale ambao walitangulia kuomba huduma hiyo ya umeme.

Comments