
Wazalishaji wa Chunvi wa eneo la Shengejuu Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba wametakiwa kuhakikisha Chunvi wanayo zalisha wanaitia madini joto kabala ya kumuzia mfanya biashara na kumfikia mtumiaji ili iwe salama kwa afya za watumiaji huko majumbani kwao .
Ili kuweza kuepuka madhara yatokanayo na utumiaji wa
chunvi ilokosa madini joto ni jukumu la kila mzalishaji wa chunvi kutia madini
joto mara tu baada ya kukausha kabla ya kuipeleka kiwandani ama kuipeki
kwenye mifuko maalumu ya kuhifadhia.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa kitengo cha lishe
Pemba Raya Mkoko Hassan wakati alipokuwa akitoa mafunzo kwa wazalishaji
chunvi huko Shengejuu eno la Ambasha Wilaya ya wete.
Alisema kutokana na tamko la serikal kwamba madhara
yatokanayo upungufu wa madini joto ni tatizo kubwa kwa Tanzania ambapo asilimia
35 ya wanawake walio kwenye umri wa kuzaa wako kwenye hatari ya kuzaa watoto
wenye mtindio wa ubongo na kupata ulemavu wa kudumunwa viuongo mbali mbali
mwilini.
Mkuu huyo wa kitengo alisema ili kumaliza kwa tatizo
hilo ni kutumia chunvi yenye madini joto kila siku .
“Wazalishaji wa chunvi munatakiwa kuwa na uwaminifu
kwenye kazi ya uzalishaji wa chunvi tieni madini joto kwani baadhi ya chunvi
hazina”.alisema Mkuu huyo.
Akitaja sheria Chini ya Mamlaka ya Chakula na Dawa
ya mwaka 2003 sura 219,ya kanuni namba 122(1)(c) ya mwaka 2010 imeweka kwa
wazalishaji na wauzaji wa chunvi kuzalisha na kuingiza chunvi yenye madini
joto.
Akizungumzia njia ya uchangaji wa chunvi na madini
joto alisema mtu anatakiwa kutayarisha rundo la tani 3 ya chunvi safi ya
mawe iliyokauka ni sawa na mifuko 60 ya kilo 50 au tani sita za chunvi laini
ambayo ni sawa na mifuko 120 ya kilo 50.
Hata hivyo aliwataka wazalishaji hao hao kupima
gramu 240 za maduni joto na kuchanganya kwenye lita 20 za maji barid yasiyokuwa
na chumvi kwenye ndoo hapo itakuwa salama chunvi hiyo .
“Jitahidini kufata maelekezo tuanayokupeni
wazalishaji chunvi ili kuepuka madhara kwa watumiaji pamoja na kufungiwa nyie
wazalishaji”. alisema.
Nae Asaa Ali Hamad, mzalishaji wa chunvi huko Shenge
juu eno la Ambasha alisema baada ya kupat Elimu hiyo ya kitalamu wataweza
kufanya biashara zao kwa uhakika zaid.
Alifahamisha kwamba iwapo mkulima wa chunvi ataweza
kufata taratibu wanazopatiwa na watalamu wao wanatapiga hatua kimaebdeleo.
Akizungumzia mafankio alopata tangu kuanza kwa kazi
hiyo ameweza kujenga nyumba ya makaazi na kuishi bila ya kumtegemea mtu na
kuweza kuajiri wafanyakazi wa kuzalisha chunvi huko kwwnye mabwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kanda anae simamia
shughuli za uzalishaji chunvi huko Shengejuu zoni (A) Hamad Omae Salum ,
alisema eneo lake lina Viwanda 22 vya uzalishaji Chunvi vilivyo
sajiliwa na mamlaka husika.
Akitaja ugumu wa kazi hiyo kwa baadhi ya wakati
nipale wakulima wake wanapo hitaji madini joto kutopata kwa wakati kutoka
na masafa ya maeneo yao kuwapata kwa urahisi.
Comments