
Afisa Mdhamini wa
Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Pemba Massoud Ali Muhammed, amewataka Wakuu wa maidara na taa sisi
zilonje ya Wizara yake kuandaa ripoti ya kazi ya Utekelezaji wa kazi kwa
kipindi cha mwaka 2017 na 2018 kuanzia mwez wa nane hadi Disemba
ambazo wamezifanya kwa kutekeleza ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015
hadi 2020 .
Uwandaaji wa ripoti hizo kwa kipindi cha miaka
miwili zita somwa katika majumuoisho baada ya kumaliza ziara ya rais wa
Zanzibar Dk Ali Muhammed Shein , ambaye anatarajiwa kufanya ziara
hiyo wiki inayofatia kisiwani Pemba.
Kauli hiyo ameitoa huko ofisni kwake wakati
alipokuwa akizungumza na Wakuu na Maidara na baadhi ya taasisi zilizo
njee ya Wizara yake ambazo zina jitegemea .
Alisema taarifa hizo zitaweza kueleza utkelezaji wa
kazi zao ambazo zimefanywa na idara ama taasisi
ambazo zimezwa kuyatekeleza kwa misingi ya ilani ya Uchaguzi kama ilivyo
ahidi kuwafanyia maendeleo wananchi wake kama walivyo ahid wakati wa
kambeni za uchaguzi kwamba wataitumia ilani hiyo kwa kulete huduma
nchini.
Viongozi wakati wa Uchaguzi waliahidi
kuwatumikia wananchi wake huduma za maendeleo zilobora kwa ilani
hiyo .
“ Wakuu wa maidara pitieni kifungu kimoja
baada ya kimoja na utekelezaji ambapo itaweza kufahamika na pale penye
mspungufunkuganyiwa marekebisho mapema”. alisema Mdhamuni huyo.
Aidha alisema kuwa Utekelezaji wa ilani ya CCM
ya Uchaguzi sio kufanya siasa kwani ndio inayowaongoza kufanya shughuli
za maendeleo ikiwemo Mkuuza na mambo mengine ya maendeleo kwa lengo
la kuwatumikia wananchi.
“Ilani ya Uchaguzi ndio mkataba wao ulowafunga
kutekeleza kwa vitendo na hili sio la Wizara moja tu ni kila Wizara inatakiwa
kufuta kwa katiba ,sheria ,utumishi wa Umma na Utawa bora bila ya
kuathiri mipango kazi yenu” .alifahamisha.
Hata hivyo Mdhamini huyo alisema kuwa wakuu wa idara
na taasisi za serikali wasione tabu kuiyelezea ilani ya Uchaguzi na kuitumikia
kwenye mipango kazi yao.
Aliwahimiza wakuu wa maidara hao siku ya
Uwasilishwaji wa ripoti ya Utekeleza wa kazi zilizofanywa kuwepo siku
hiyo ili kuweza kuichangia pale patakapokuwa na mapungufu .
Kwa Upande wake afisa Mdhamini wa tume ya maadili
Pemba Hanuna Ibrahim Massoud, alisema uandaji wa ripoti hizo ni muhimu
kutayarishwa mapema ili kuweza kupitiwa na kuangaliwa ikiwa kuna mapungufu
kufanyiwa marekebisho kwa wakati.
Hata hivyo alifahsmisha kuwa uwandaaji wa
ripoti hizo sio wa mtu mmoja unahitaji kushirikiana kwa pamoja ili
kuweza kuyaelezea yale yalotekelezwa ndani ya ilani ya
Uchaguzi CCM ya Mwaka 2015 /2020 .
Hata hivyo Mdhamini huyo aliwaomba wakuu hao wa
maidara kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu katika wizara yake
anayoifanyia kazi kwa sasa.
Kwa upande wake Mdhamini wa ofisi ya Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali Said Khamis Juma ,alisema ili kufanya vyema
majukumu ya kazi zao ni kuitekeleza ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ambayo
ndio katiba ya shughuli za maendeleo na mipango ya nchi.
Hata hivyo aliwaomba wakuu wamaidara waloshiriki
mkutano huo kumpa ushirikiano wa kazi zake ndani ya ofisi kwani ameshika nafasi
hiyo baada ya mabadiliko yalofanyika hivi karibuni .
Wakuu wa maidara alizozungumza nazo ni
Tume ya Maadili, Mahkama ,Chuo cha Utumi wa Umma Ipa Pemba , Mamlaka ya kuzuia
rushwa ,Ofisi ya Mufti na Ofisi Mdhibit Mkuu wa hesabu za serikali Pemba .
Comments