Wananchi wa Wilaya ya Micheweni wameshauriwa kuwa na
tahadhari juu ya utendaji wa shughuli zao za kimaendeleo kwa kuhakikisha wanaweka miundombinu itakayosaidia uokozi
pindi maafa yanapotokea.
Mkuu wa wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib ametoa
ushauri huo katika mafunzo juu ya uwelewa wa kukabiliana na maafa kwa wananchi
wa Micheweni yaliyoendeshwa na kamisheni
ya kukabiliana na maafa Kisiwani Pemba .
Mkuu huyo amesema
jamii inawajibu wa kufuata taratibu za ujenzi uliosalama na kuweka usafi
wa mazingira ili kuwa rahisi kujikinga na
majanga hayo .
Awali Kaimu mratibu wa kamisheni ya kukabiliana na maafa
Pemba Mbela Issa Mbela amesema wilaya ya micheweni imekuwa na uzoefu wa kutokea
maafa kutokana na mazingira yake kukabiliwa na ukame wa mara kwa mara.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema licha ya
kuwepo elimu za mara kwa mara bado kuna maeneo hasa ya visiwa vidogo vidogo
yameanza kuleta ishara ya kutokea maafa na tahadhari inapaswa kuchukuliwa .
Shehia zilizopatiwa mafunzo hayo ni pamoja na Msuka
magharibi, Tumbe magharibi na Shumba
mjini .
Comments