WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imetaifisha mali za Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) zenye thamani ya sh bilioni 118 zilizokuwa zinamilikiwa na watu kinyemela kisha kuzirejesha serikalini ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya Serikali ya awamu ya tano ya kulifufua shirika hilo.
Zoezi hilo limefanyika katika kipindi cha ndani ya siku 30
Pia Serikali inaendelea na uhakiki wa mali hizo popote zilizopo ambazo nazo zote zitarejeshwa ili kuwezesha shirika hilo kuanza kazi baada ya menejimenti yake kuundwa mwishoni mwa mwaka jana.
Akijibu hoja za wabunge kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Maji bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina Serikali ya awamu ya tano iko kwenye hatua za mwisho za kulifufua shirika hilo.
Pia Serikali inajiandaa kununua meli mbili kubwa ambazo zifanya kazi ya uvuvi katika ukanda wa uchumi wa bahari kuu ilikukidhi matakwa ya wabunge ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiitaka Serikali kuwekeza kwenye ukanda huo.
Aidha Waziri Mpina alisema tayari Serikali ya Japan imeshaahidi kutoa sh bilioni 4.3 kwaajili yakufufua miundombinu ya Shirika la Uvuvi ikiwemo majokofu ya kuhifadhi samaki, gari la barafu, meli moja ya uvuvi nakujenga gati la kuegesha meli za shirika hilo.
“Kumekuwa na kilio cha wabunge cha miaka mingi kutaka Serikali iingie kwenye uvuvi wa bahari kuu,nataka kuwahakikishia Serikali ya awamu ya tano tunaingia kuvua kwenye uvuvi wa bahari kuu na mipango iko vizuri”alisema Mpina
Kuhusu ujenzi wa bandari ya Uvuvi, Waziri Mpina alisema tayari mtaalamu mwelekezi anaendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na kwamba mara baada ya kukamilika kazi hiyo ujenzi wa bandari ya uvuvi utaanza .
Waziri Mpina amesisiti za kuwa mbali nakulifufua shirika la uvuvi, Serikali ya awamu ya tano inakwenda kufufua viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo nakujenga vingine vipya katika maeneo mbalimbali nchini.
“Hivi sasa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata mazao ya mifugo kinakwenda kujengwa eneo la Ruvu ambacho kitakuwa na machinjio ,kitasindika nyama, kitasindika ngozi, kitasindika mazao ya ngozi ukiingiza mfugo unatoka na kiatu”alisema Mpina
Alisema, tayari Wizara imefanya mkutano tarehe 5/2/2019 na ujumbe wa Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri Mheshimiwa, Dkt Ezzidine Abu Stiet, ulioongozwa na Balozi wa Misri nchini Mheshimiwa, Mohammed Gaber Abdulwafa.
“Tumekubaliana kuwa, utiaji wa saini mkataba huo utafanyika tarehe 24/2/2019 hapa nchini. Baina ya Kampuni ya Ranchi za Taifa(NARCO) kwa upande wa Tanzania na Kampuni ya Uwekezaji kwa Nchi za Afrika ya nchini Misri ijulikanayo kama “The National Egyptian Company for Africa Investment” (NECAI) kwa niaba ya Serikali ya Misri” alisisitiza
Pia Serikali itaanza ujenzi wa mnada wa kimataifa wa mifugo Ruvu na kwamba tayari wamekutanana Waziri waMifugo wa Misri kukubaliana ujenzi wa kiwanda hicho uanze Machi mwaka huu.
Vile vile viwanda vingine vya kuchakat amazao ya mifugo vinajengwa Longido, Tan Choice Kibaha chenye uwezo wa kuchinja ngombe zaidi 1,000 na mbuzi 4,000 nakiko kwenye hatua ya mwisho kukamilishwa huku Kampuniya KOMU ya Kahama nayo ikiwa kwenye hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa kiwandaChato
Hivyo Serikali ya awamu ya tano iko kazini matatizo ya wananchi kukosa soko la mifugo sasa yamefika mwisho kwani wafugaji wengi watapata masoko ya uhakika ya mifugo yao hapanchini.
Kuhusu huduma za mifugo, Waziri Mpina alisema zoezi la uogeshaji wa mifugo ambao lilisimam akwa muda mrefu lakini kwasasa Serikali ya awamu ya tano inaogesha mifugo kila kona ya nchi na tayari wizara imegawa dawa kwenye majosho yote 1, 409 yanayo fanyakazi na kwamba wizara itaendelea kutoa dawa kwa ajili ya uogeshaji.
Alisema wafugaji walikuwa wanateswa kuogesha ng’ombe mmoja sh 2,000 lakini sasa hivi watakuwa wanachangia gharama ndogo kwa kila ng’ombe sh 50 tu.Kuhusu operesheni za kulinda rasilimali za mifugo na uvuvi, Waziri Mpina alisema wabunge wameishauri Serikali kuhusu uwekezaji wa viwanda lakini Serikali inawajibu wa kuwalinda wawekezaji wa ndani.
“Tunazungumza uwekezaji, leo hivin ania nayeweza kuja kwenye uwekezaji kwenye nchi ambayo haiwezi kulinda rasilimali zake, na ni atakayejenga kiwanda hapa cha kusindika samaki wakati samaki wote wanatoroshwa kwenda nje ya nchi bila hata kufuata utaratibu unaokubalika ni nani”alihoji Waziri Mpina,
“Nani leo atakayekubali kuwekeza kuzalisha vifaranga, kuku, ngombe wa maziwa katika nchi ambayo maziwa yanatoka nje ya nchi hayana vibali hayajalipiwa kodi yoyote, hayajapimwa ubora na yanauzwa na yanashindana na viwanda vya ndani nani atakayejenga viwanda hapa nchini”alihoji.
Pia Waziri Mpina alisema nani atakayejenga viwanda katika nchi ambayo inaruhusu mpaka vitu vilivyoisha muda wa matumizi kuuzwa nchini na kushindana na wazalishaji wa ndani nani atakubali.
“lazima tukubali doria zinazoendelea zinalenga kuwalinda wazalishaji wandani ili waweze kuzalisha vizuri leo nenda kawaulize wazalishaji wa viwanda vya maziwa wameamua kuongeza uzalishaji kwasababu kuna ulinzi madhubuti hakuna mtu ataingiza kimzahamzaha maziwa kutoka nje ya nchi”alisema Mpina.
Aidha Waziri Mpina alisema katika vitu ambavyo alivichukia kuliko vyote miaka ya nyuma niwatu kuleta vitu vilivyokwisha muda wamatumizi ambao wamepita njia za panya alafu waziri mhusika anakuja bungeni nayeye analalamika juu ya mambo hayo.
“Wakati yeye ndio anauwezo wakuwashika, sisi tutawashika na hatutakubali kuruguza wawekezaji wetu hapa nchini”alisema.
Hivyo aliwaomba wabunge kuunga mkono juhudi za Serikali za kulinda rasilimali hizo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote kwani rasilimali hizo zikitoweka hata wao hawawezi kunufaika.
Hivyo aliwaomba wabunge kuunga mkono juhudi za Serikali za kulinda rasilimali hizo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote kwani rasilimali hizo zikitoweka hata wao hawawezi kunufaika.
“Nani anaye wahurumia wavuvi ni mtu ambaye anaruhusu watu wakavue kwa nyavu haramu alafu baadae mvuvi anaenda kuvua kwa gharama kubwa anarudi bila samaki au ni yule anayelinda mwisho wavuvi wa kienda kuvua wakarudi na samaki wengi ili wawe matajiri nani anayewatetea wavuvi na huo ndio msingi hasa doria hizo”alisema Mpina.
Mpekuzi.
Comments