Zitto Kabwe Kuweka Hadharani Majibu Aliyojibiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) Kuhusu Sakata la CAG Kuhojiwa na Bunge.
Mbunge
wa Kigoma Mjini, (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, ameahidi kuwa leo
ataweka hadharani majibu aliyopatiwa baada ya kuandika barua kwa Katibu
Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA).
Zitto
aliandika barua hiyo akipinga hatua iliyochukuliwa na Spika wa Bunge,
Job Ndugai kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),
Prof. Mussa Assad kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya, Kinga na Haki
ya Bunge kuhojiwa.
Mbunge
huyo na Kiongozi Mkuu wa ACT- Wazalendo, aliwatumia barua hiyo maspika
wa mabunge yote ya Afrika kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola,
Wadhibiti na Wakaguzi Wakuu wa Hesabu za Serikali wa Afrika katika nchi
wanachama wa Jumuiya ya Madola pamoja na wale wa nchi za Jumuiya ya Nchi
Kusini mwa Afrika (SADC).
Hatua
hiyo imekuja baada ya Spika Ndugai kumtaka Prof. Assad kufika mbele ya
kamati hiyo Januari 21, mwaka huu, kujieleza kuhusu kauli yake aliyoitoa
akiwa nchini Marekani kuwa ‘Bunge ni dhaifu’.
Kwenye
barua hiyo aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii, Zitto alieleza kuwa amewaomba viongozi hao waongee na Spika
Ndugai ili aachane na uamuzi wake wa kumwita CAG kuhojiwa na Kamati ya
Bunge.
Sehemu ya barua hiyo aliyomwandikia Katibu Mkuu wa CPA, Akbar Khan, ilieleza:
“Kwa
kuwa Bunge la Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Madola, naiomba
ofisi yako ifanye mawasiliano ya kidiplomasia kwa kuwasiliana na Spika
wa Bunge la Tanzania kumweleza hatari ya uamuzi anaotaka kuuchukua,”
alisema na kuongeza:
“Ninaamini
suala hilo linaweza kumalizwa kwa ustaarabu na kuimarisha uhusiano kati
ya taasisi hizo mbili, yaani Bunge la Tanzania na Ofisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambao wote wanategemeana katika
ufanyaji kazi,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.
Mpekuzi.
Comments