Wizara ya Elimu Zanzibar yawataka wamili wa vyuo kufanya udahili katika taasisi zao.

Image may contain: 1 person, sitting
Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Mhe Riziki Pembe Juma amewataka wamiliki wa vyuo na wadau wa Elimu Zanzibar kuhakikisha wanafanya udahili wa Taasisi zao kwa kufata utaratibu uliowekwa na baraza la Elimu ya Sayansi na Ufundi NACTE.

Akifungua mkutano wa Baraza hilo na wakuu wa vyuo mbalimbali wa Taasisi za Sayansi na ufundi katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Mazizini Unguja udahili wa Vyuo au Taasisi utasaidia kuondosha tatizo la vyuo hewa na kupunguza wimbi la wahitimu wasio na sifa.

Amefahamisha kuwa kufanya udahili pia kutawasaidia wadau hao kuondosha tatizo la wahitimu kutokua na namba ambazo zitawaruhusu wanafunzi kuendelea mbele katika masomo yao yani AVN namba.

Hata hivyo Mhe. Riziki amewasisitiza watendaji wa Nacte kuondosha muhali kwa vyuo au taasisi za Elimu zinazoendelea kufanya usaili wa wanafunzi wapya wakati taasisi au vyuo hivyo havina sifa ya kuendesha kufanya hivyo kwani inawatia hasara kubwa wazazi pamoja na kuwapotezea muda vijana waliojisajili.

Nae katibu mtendaji Baraza la Elimu ya Sayansi na ufundi Dkt.Adolf Rutayuga amesema ni jukumu la Nacte kuwafahamisha wakuu wa taasisi hizo kufata taratibu za usajili wa taasisi zao pamoja na kupitia mitaala yote ya vyuo hivyo ili kuondoa tatizo la wahitimu hewa.

Nao washiriki wa mkutano huo wameiomba Nacte kuongeza mashirikiano na taasisi hizo ili kuweza kuondosha matatizo yaliopo baina ya wamiliki wa vyuo na Nacte.

Comments