Akizungumza baada ya kufungua kituo kipya cha afya cha
Kiuyu Kipangani kiliopo Wilaya ya Micheweni Pemba, ikiwa ni shamra
shanra za maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe Riziki
amesema Serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi katika kutoa
huduma mbalimbali ikiwemi afya kama ilivyoahidi katika ilani yake, hivyo ni lazima kuthamini juhudi hizo.
Amewataka waanchi kukitumia kituo hicho katika kupata huduma mbalimbali
za afya hasa kina mama kwa kujifungulia ndani ya kituo hicho badala ya
kujifungulia majumbani, ili linapotokea tatizo liweze kutatuliwa kwa
haraka na kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.
Aidha amewataka akina baba kuwasimamia akina mama juu ya suala hilo la kutojifungulia majumbani pamoja na kuwaunga mkono wakati wanapokwenda kliniki ili kujua matatizo waliyonayo na kuwasaidia.
Aidha amewataka wataalamu wa afya kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa wao na kutowanyanyapaa, kwani kazi hiyo ni ngumu na inahitaji upendo na pia kuacha tabia ya kuwachangisha wananchi kwani huduma za matibabu ya afya ni bure.
Pia amewataka kuvitunza vifaa tiba ili viweze kutumika kwa muda mrefu kwani vina gharama kubwa, na kuwatahadharisha wenye tabia ya kuviuza vifaa hivyo au dawa na ataebainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Hata hivyo amewashukuru washirika wa maendeleo Serikali ya Uholanzi chini ya kitengo chake cha ORIO pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa juhudi walizochukua kwa kujenga kituo hicho katika hali ya ubora zaidi pamoja na kuweka vifaa vya kisasa.
Akisoma taarifa juu ya ujenzi wa kituo hicho cha afya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya bi Halima Maulid Salum amesema ujenzi wa kituo hicho ni miongoni mwa vituo 15 vilivyojengwa kwa unguja na Pemba, ambapo ni miongoni mwa matunda ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Comments