Waziri wa Elimu Zanzibar asema wizara yake imefanikiwa kutekeleza maagizo ya Rais.

Image may contain: 1 person, outdoorWAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma amesema wizara yake imefanikiwa kutekeleza maagizo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein katika kujenga madarasa ya skuli katika maeneo mbalimbali Unguja na Pemba.

Akizungunza wakati alipomkaribisha rais wa Zanzibar kuzungumza na wananchi baada ya kufungua Skuli ya Msingi Chimba, iliyopo Wilaya ya Micheweni, ikiwa ni shamra shamra za Sherehe za kutimiza miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe Riziki amesema walitakiwa kufanya hivyo bila ya kujali itikadi za kisiasa au kitu chochote.

Amesema kuna mafanikio makubwa yamepatikana katika uongozi wa Dr. Shein ambapo amewataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo ili kupata maendeleo zaidi.

Amesema lengo la kujenga madarasa hayo ni kuwapunguzia watoto kufata elimu masafa ya mbali pamoja na kuwafanya kupata elimu bora.

Skuli ya msingi Chimba imejengwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha chimba, mfuko wa jimbo wa Mwakilishi na Mbunge pamoja na Halmashauri na ina madarasa manne na ofisi za walimu mbili.Image may contain: 1 person, standing and outdoor

Comments