WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amefungua mradi wa maghala ya kuhifadhi nafaka na
soko la mazao la OTC-Lilambo katika Halmashauri ya Songea uliogharimu
sh. bilioni 1.5.
Amesema
Rais Dkt. John Magufuli ameazimia kuwawezesha wakulima kuwa na mahala
pa uhakika pa kuhifadhia mazao yao na sehemu ya kufanyia biashara ili
kuwaongezea tija.
Amefungua
soko hilo jana (Alhamisi, Januari 3, 2019) akiwa katika siku ya pili
ya ziara yake ya kikazi ya siku nne ya kukagua shughuli za maendeleo
mkoani Ruvuma.
Waziri
Mkuu amesema ameridhishwa na ujenzi wa soko hilo pamoja na maghala
kwani umezingatia viwango. Maghala hayo mawili yana uwezo wa kuhifadhi
tani 5,000 za nafaka.
“Licha
ya soko hili kuwapa wakulima wetu fursa ya kupata masoko ya kuuzia
mazao yao, pia watapata mafunzo ya namna ya kuhifadhi bidhaa zao pamoja
na taarifa za masoko.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu ameiagiza bodi ya soko hilo kuhakikisha inatoa matangazo
katika vyombo mbalimbali vya habari ili wakulima waweze kupeleka mazao
yao sokoni hapo.
Wakati
huo huo, Waziri Mkuu amewataka wananchi kutumia vizuri mvua
zinazoendelea kunyesha nchini kuandaa mashamba, kupanda mazao mbalimbali
ya chakula na biashara.
“Nawaagiza
viongozi wa kata na vijiji hakikisheni wananchi katika maeneo yenu
wanaandaa mashamba na kupanda kwa wakati, tunataka tuwe na chakula cha
kutosha na ziada tuuze.”
Awali,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songea, Martin Mtani ameiomba
Serikali iwapatie mashine itakayowawezesha kupanga madaraja ya mazao ya
nafaka mbalimbali.
Mkurugenzi
huyo ameomba soko hilo liwekwe kwenye mpango wa kujengewa vihenge
vyenye uwezo wa kukausha mazao kwa viwango vya kimataifa ili kutatua
tatizo la unyaufu.
Pia
Mkurugenzi huyo ameiomba Serikali iwasaidie katika kuliunganisha soko
hilo na TMX ili waweze kuuza mazao ya nafaka ndani na nje ya nchi .
Ufunguzi
huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Ajira na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama na Waziri wa Kilimo Japhet
Hasunga.
Wengine
ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dkt. Damas Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na maafisa
wengine wa Serikali.
Mpekuzi.
Comments