Waziri wa Madini, Doto Biteko jana Januari 28, amekutana na Mzee Eric Mchata na Kampuni ya madini ya Uranium ya Mantra Tanzaniakwa lengo la kutatua mgogoro uliopo baina ya pande hizo mbili.
Kikao hicho, kinafuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Januari 22 na Mzee Mchata wakati wa mkutano wa Kisekta ulioshirikisha wachimbaji wadogo na wadau wa madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wakati akisikiliza kero za wachimbaji na wadau wa madini walioshiriki kikao hicho, Rais Magufuli alipokea kero ya Mzee Mchata aliyemweleza kwamba amekuwa na mgogoro na kampuni hiyo kwa kipindi cha takribani miaka 12 na bado hajapata suluhu.
Akijbu kero iliyowasilishwa na Mzee Mchata, Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Madini kuhakikisha mgogoro huo unafikia mwisho.
Mpekuzi.
Comments