Wamiliki wa vituo vya mafuta wakubushwa juu ya usalama wao.


Image result for vituo vya mafuta
Wamiliki wa vituo vya mafuta  Kisiwani Pemba wametakiwa kuwa na mpango maalum wa kujiwekea miundombinu  bora ya usalama kwenye sehemu zao ili kuwa rahisi kujiokoa pindi kunapotokea maafa .

Wameshauriwa kuwapa mafunzo wafanyakazi wao pamoja na kutenga vifaa vya huduma ya kwanza ili kuwa na uwezo wa kujisaidia wenyewe kabla ya kutokea athari zaidi .

Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na Mkuu wa Operation ya kukabiliana na maafa Zanzibar Shaaban Hassan Ramadhan katika ziara ya ukaguzi wa bohari na vituo vya mafuta kisiwani humo.

Amesema katika ukaguzi huo wamegundua mapungufu mengi ya kiusalama huku akitoa agizo la miezi mitatu kwa wamiliki kuyafanyia kazi mapungu hayo kabla ya kutokea maafa yasiyotarajiwa .

Katika ziara hiyo mkuu wa operation ya uokozi kutoka kikosi cha zimamoto ali abdi hashim amesema baadhi ya vituo havina dawa mitungi ya kisasa ya kuzimia moto wala matangi ya maji hivyo kuwa vigumu kwao kuweza kujiokoa .
Nao baadhi ya wasimamizi wa vituo hivyo vya mafuta wamesema watayafanyia kazi mapungufu madogo madogo yaliopo na yale makubwa watawasiliana na wamiliki wao kwa ajili ya hatua .

Comments