
Tamwa imeomba kuendeleza
mradi wa PAZA ili matatizo yalio ibuliwa yamalizike.
Hayo yameelezwa na Bi
Salma Ali Hamadi miaka (50) kufatia
kuepo kwa tatizo la ujenzi wa uzio katika skuli ya Muungoni ambalo
halijatekelezwa wananchi wa muungoni wameshindwa kujua sababu ya kutojengwa kwa
ujenzi wa uzio huo .
Amesema Mradi wa PAZA
umewawezesha wananchi wa Muungoni kuhamasika na kuweza kufuatilia njia za
kutatua matatizo mengi ikiwemo tatizo la uchakavu jengo la afya ambapo
limeboreshwa na huduma zinapatikana ipasavyo hospitalini hapo.
Wakizungumzia huduma ya maji safi na salama wakaazi wa shehia ya Muungoni wilaya ya
Kusini Unguja wamesema huduma hio imepatikana baada ya kupata mashine
mpya ya kuvutia maji katika kisima kutokana na kuhamasika na Mradi wa kukuza uwajibikaji
Zanzibar (PAZA) unaosimamiwa na chama cha waandishi wahabari wanawake
Zanzibar(TAMWA-ZANZIBAR).
Aidha amesema mradi huo
umesaidia kuwaletea visima vya maji safi na salama ingiwa maji hayo
yanachumvi kidogo lakini umeweza kuwaondolea tatizo sugu la maji kutokana na
huduma hiyo kuwa muhimu katika jamii.
.
Sambamba na hayo
amewashukuru watendaji kazi wa ofisi ya Halmashauri za wilaya kwa namna
walivyowajibika katika kutekeleza majukumu yao kwa wakati na wananchi
wameridhirika kwani tatizo la maji lilikua kubwa.
Kwa upande wa Asasi za
kiraia na matandao wa Ardhi wilaya ya kusini, Halda Nassor Haji ambae
anawahamasisha waakazi wa shehia ya Kitogani na Muungoni amesema watendaji wa
Halmashauri wameshafanya tathmini ya ujenzi wa uzio katika skuli hiyo lakini
bado halijatiwa katika utaratibu wa mpango wa matumizi ya kifedha(bajeti)
.
Hivyo amewaomba wananchi
waendelee kuwa wavumilivu na endapo ujenzi wa uzio, huo utakapokua tayari
watapewa taarifa .
NA RAHMA MOH’D.
Comments