Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeiomba mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu kwenda gerezani kumhoji mshtakiwa wa pili Alloycious
Mandago katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh2bilioni.
Wakili
wa Takukuru Leonard Swai ameeleza hayo jana Alhamisi, Januari 24, 2018
mbele ya hakimu mkazi mkuu Thomasi Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa
ajili ya kutajwa.
Swai
alidai kesi hiyo iko hatua za mwisho kwa ajili ya kuandaa maelezo
lakini wanaombi kwa ajili ya kumhoji mshtakiwa wa pili akiwa magereza.
Mahakama
iliridhia mshtakiwa huyo kuhojiwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi
Februari 8, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Mbali
na Mandago, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara
Mohamed Yusufali na Isaac Kasanga ambao kwa pamoja wanakabiliwa na
mashtaka 39 likiwemo la kuisababishia serikali hasara ya Sh2 bilioni.
Mpekuzi.
Comments