Waziri wa elimu Zanzibar asema kutowa mafunzo ya Amali ni gharama.

Image may contain: 2 people, people standing
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema inatambua kuwa kutowa mafunzo ya Amali ni gharama, kwani yanahitaji vifaa vya kisasa, walimu wenye ujuzi unaoendana na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia.

Akizungumza katika sherehe ya kukabidhi vifaa vya kuimarisha kazi za vitendo kwa vituo vya mafunzo ya Amali vya watu binafsi na Taasisi nyengine za Serikali leo, Waziri wa Elimu na Matunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma amesema kwa uelewa huo ndio imeamua kuanzisha mfuko wa kodi ya maendeleo ya ujuzi ili kusaidia upatikanaji wa vifaa hivyo kwa lengo la kuzalisha tena wataalanu katika vyuo mbalimbali.


Amesema mamlaka ya mafunzo ya Amali ni moja ya wanufaika wa mfuko huo, na katika jukumu lake la kusimamia Mafunzo ya Amali nchini ni pamoja na kutoa ufadhili kwa vituo binafsi kupitia kodi ya kuendeleza ujuzi.

Aidha ameviomba vituo ambavyo vimepatiwa ufadhili wa vifaa hivyo kutokana na kutimiza vigezo na masharti yaliyowekwa, ni vyema kuongeza ari ya kuwafundisha vijana kitaalamu zaidi yanayoendana na soko la ajira ili vijana watakapo maliza waweze kujiajiri na kuajiri wengine ikiwa ni lengo la Serikali la kupunguza tatizo la ajira na umasikini liweze kufikiwa.

Hata hivyo amevitaka vituo vyengine vya mamlaka ya mafunzo ya Amali kutimiza masharti yaliyowekwa ili nao waweze kunufaika na ufadhili kama huo amabapo amesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali ili kuona vituo vya Mafunzo ya Amali vinaimarishwa kama ilani ya CCM ya 2015 inavyoelekeza.

Akisoma risala yao kwa niaba ya vituo waliokabidhiwa vifaa hivyo,Mrajis wa Kituo cha Mwenge ndugu Abubakar Mwadini Hassan, wamesema kupatiwa vifaa hivyo bure kunaonesha wazi ni maendeleo ya mapinduzi ya mwaka 64 katika kuhakikisha elimu bure inapatikana kwa wote.

Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzi ya Amali Zanzibar bw Bakari Ali Silima amesema matatizo yanayo vikabili vituo vya mafunzo ya Amali ni pamoja na baadhi ya vituo kwa muda mrefu kutokuwa na usajili hata wa muda ambao hutakiwa kutimiza vigezo ili kupata usajili wa kudumu.

Jumla ya vituo vinne vimekabidhiwa vifaa mbalimbali ikiwemo, Mwenge Community centre,Kituo cha mafunzo Karume, Melisha Training centre na Adalt training centre ambapo wamekabidhiwa vifaa mbalimbali ikiwemo vyarahani, mashinr ya photocopy, mafriji, pamoja na vifaa vya Ufundi wa umeme.Image may contain: 2 people, people standingImage may contain: 7 people, people sitting

Comments