Akitoa taarifa za matukio ya wiki ofisini kwake Mwembemadema, Kamanda
wa Polisi Mkoa huo, Thobias Sodayka, aliwataja marehemu hao kuwa ni
Alex Markus Silanpaa (35) raia wa Finland na Rashid Juma Hamad (35) wa
Welezo.
Alisema, tukio la Alex lilitolea Januari 4 mwaka huu ya saa10:40 jioni katika gesti hiyo.
Aidha alisema taarifa za kifo cha mgeni huyo zilipatikana kutoka kwa
Ali Salim Buheti (53) mkaazi wa Malindi ambae alitilia shaka kuwa katika
gesti hiyo chumba namba tisa kuna mtu amefariki na askari walipokwenda
walikuta maiti yake.
Alisema chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana huku mwili wa
marehemu ukihifadhiwa katika hospitali ya Mnazimmoja kwa uchunguzi.
Akielezea kifo cha Rashid Juma Hamad (35) mkaazi wa Welezo, alisema
kijana huyo alifariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya
Mnazimmoja baada ya kupigwa na watu aliowataja kuwa askari wa JKU.
Alisema tukio hilo lilitokea Januari 3 mwaka huu saa 10:30 usiku maeneo ya Amani.
Alisema chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuwa marehemu na wenzake walituhumiwa kumkaba DJ kwa lengo la kufanya unyanganyi.
Hata hivyo, alisema wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo ili kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wahusika.
Aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo na kutoa taarifa za matukio ya uhalifu ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Comments