Paza yazidi kufanya vyema kupitia huduma za afya.



Afisa Afya wa wilaya ya kusini Jaku Ameir Issa amesema ofisi yao inaendelea kusimamia huduma za afya ili kuhakikisha wanawake wa mkoa huo wanapata huduma za Afya ya Uzazi bure kwa kupatikana  madaktari wakutosha katika wila hiyo.

Ameyasema hayo kupitia Mradi wa kukuza Uwajibikaji Zanzibar (PAZA) unaosimamiwa na Chama Cha wa Waandishi wa Habari wanawake Zanzibar (TAMWA- ZANZIBAR). Amesema wakaazi wa kijiji cha Kitogani wamehamasiki kuibua matatizo mbalimbali  kupitia   mkutano mkuu wa kijiji ambao uliwashirikisha wananchi wa kijiji cha Kitogani  kwa lengo la kuibua changamoto zinazo wakabili kijijini hapo.

Akifafanua miongoni mwa changamoto zilizokuwa zikiwakabili  ambazo zimetatuliwa kupitia mradi  wa (PAZA) kwa kuboreshwa hospitali ya Kitogani ambapo jengo la hospital hiyo lilikua limechakaa sana  pamoja ukosefu wa madaktari.

Hata hiovyo  amesema jumla wa watu wenye ulemavu 33, wanawake 42 na vijana 18 walifika ofisini kwake kupeleka maombi ya malalamiko ya kuomba kuboreshwa  huduma ya afya.


Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji wa kitogani Bi Khadija Kheiri mwenye umri wa miaka (58) amesema PAZA imetusaidia kupata huduma ya  maji safi na salama , jengo la hospitali limejengwa vizuri ingawa hatujakabidhiwa lakini limeshafanyiwa ukarabati mzuri limependeza.

Khadija amesema wananchi wa Kijiji cha kitogani walikuwa wamekabiliwa na matatizo mengi ikiwemo la maji safi na salama, ukosefu wa walimu, huduma ya afya pia ilikuwa mbovu.

Sambamba na hayo ameeleza kuwa Mradi wa PAZA umesaidia  kuwaelimisha  wananchi taratibu za kufuatilia  ufumbuzi wa matatizo katika  Ofisi ya Halmashauri za wilaya na kuwajua maafisa wa serikali kawaajili ya kuwajibisha katika majukumu yao.

Bi Khadija  amesema wananchi wa Kijiji cha kitogani walikuwa wamekabiliwa na matatizo mengi ikiwemo la maji safi na salama, ukosefu wa walimu, huduma ya afya pia ilikuwa mbovu.

Mradi wa kukuza Uwajibikaji Zanzibar (PAZA) ulianza mwaka jana kwa lengo la kukuza Uwajibikaji Zanzibar ili kuwahamasisha wananchi njia za kutatua matizo yanayozunguuka katika jamii na utarajiwa kumalizika  mwakani
.
Na RAHMA MOH’D

Comments