Muamko wa wananchi juuu ya mradi wa Paza waendelea kuimarika Unguja.


Wakaazi wa Kitogani  wameomba watendaji wa Mradi wa PAZA kuendeleea na mradi kutokana na  bado watu wanamuamko mdogo wa kuhudhuri mkutano wa kijiji kutokana na itikadi za kisiasa .

Akizungumza na muandihi wa habari hizi Amesema baadhi ya watu wanapoitwa kuhudhuria kwenye kikao cha kijiji wanapuunza na kuendelea na shughuli zao na hatimae kukosa taarifa za maendeleokatika maeneo yao .

Kwa upande wa wanufaika wa Mradi huo Wahida Khatib Ali mika (24) mkaazi wa Muungoni amesema kupitia mradi wa PAZA wanaelimika njia ya kuwafuata watendaji wa Halmashauri na kujua majukumu yao.

Hivyo ameeleza kuwa  ameridhishwa utendaji wa Mradi wa PAZA kwa umewaondolea matatizo mengi, wilaya ya kusini ikiwemo tatizo la utoro kwa wanafunzi, shida ya mji safi na salama, ukarabati wa vitua vya afya na majengo ya skuli.

Amesema  Wahida “ Paza imenielimsha naweza kuandika barua ya malalamiko ya shida ya maji na kupeleka Halmashauri na kufuatilia hadi kufikia hatua ya mafanikio, tulihudhuria mkutano sisi wote tunaweza kutatua matatizo yetu kwa sasa”

Nae Mwana asasi za kiraia Halda Nassor Haji miaka  (32) amesema  amewashajihisha  wanawake 100 elimu ya kukuza uwajibishaji katika shehia hizo ili waondokane matatizo katika vijijini mwao .

Amesema wametumia njia ya mkutano kuwaeleza elimu hiyo akinamama ambapo pia kila mwanakijiji alipata fursa ya kuibua matatizo yalimkabili katika eneo lake.

Ameeleza kuwa  wanaasasi wote walipewa mafuzo na chama cha waandishi wa habari wanawake Zanzibar (TAMWA-Zanzibar) kupitia Mradi wa Kukuza uwajibikaji Zanzibar (PAZA) na kuwataka elimu hiyo kuwafikishia wanawake wenzao vijijini.

Jumla wa wanawake 100 wa shehia ya Muunguno, Kitogani na Bwejuu wilaya ya kusini Unguja wamehamasikia na elimu ya kukuza Ujibikaji  Zanzibar kupitia asasi za kirai na mitandao ya ardhi ambapo elimu hiyo imewaleta maendeleo katika maakazi yao ikiwemo kuondokewa na tatizo la maji, afya na elimu.

NA RAHMA MOH’D

Comments