Mh. Riziki : walimu simamieni vyema majukumu yenu hasa katika kipindi hichi cha mitihani ya marudio Zanzibar.

Amesema utaratibu
utakaotumika Mara hii ni tofauti na ule wa mwanzo uliozoeleka, hivyo ni
vyema kuwa makini ili kuepuka matatizo yanayoweza kuwatokea.
Akizungumza na walimu hao katika skuli ya Mchangamdogo Wilaya ya Wete Mhe Riziki amewataka walimu kufuata kufuata maadili ya kazi zao na kutambua kuwa suala la mitihani ni la wote.
Aidha amewataka kushirikiana na kutoa taarifa kila watakapoona kuna
tatizo linaloweza kuhatarisha usalama wa zoezi zima la mitihani
inapoendelea kwa lengo la kufanikisha zoezi hilo.
Kuhusu kuanza kwa masomo baada ya kumaliza mitihani, Mhe Riziki amewataka Walimu Wakuu kuwafuatilia kwa makini walimu wao kwa kufundisha kwa mujibu wa vipindi wanavyopangiwa na kuacha Tabia ya kutoka ovyo madarasani bila ya kuwa na dharura maalum.
Amesema bado kuna baadhi ya walimu wamekuwa na desturi za kutoka ovyo madarasani pamoja na kufanya mazungumzo yasio na maana na kujisahau juu ya wajibu wao hali inayopelekea kutomaliza *sylubus* zao kwa wakati.
Hata hivyo amewataka kutokuwa wakali kwa wanafunzi na badala yake wawe na moyo wa kujitolea ili waweze kuwasaidia na kuweza kufaulu vyema katika masomo hao.
Pia amewataka kushajiishana kusherehekea maendeleo yaliopatikana tokea kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushiriki katika kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuwasimamia wanafunzi ili sherehe hizo zifanyike kwa amani na utulivu.
Nae Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo y Amali Zanzibar Mhe Mmanga Mjengo Mjawiri amewatahafharisha walimu wenye Tabia ya kutoa taarifa kwa watu mbalimbali juu ya Sera ya elimu bila malipo kwani hiyo sio kazi yao.
Amesema kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakieneza juu ya kutokuepo madaftari jambo ambalo si la kweli kwani Serikali imetenga shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kununulia madaftari na shikingi milioni 600 kwa ajili ya vifaa vya sayansi.
Hivyo amesema vitu hivyo vipo na wakati wowote baada ya kumalizika sherehe za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, vitagawiwa.
Aidha amewataka kuacha kuharibu taswira njema ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuendelea kutoa huduma bora za Elimu kwa wananchi wake, kwani sera ya elimu ni kielelezo cha uzalendo ,hivyo itekelezwe kwa ubora wake.

Comments