Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kutolea huduma za
kibenki na kuzima mfumo wa zamani, hafla ambayo iliyofanyika makao makuu
ya PBZ Mperani ikiwa ni shamrashamra za miaka 55 ya mapinduzi ya 1964.
Alisema hatua hiyo itawarahisishia wateja kupata huduma hizo kwa haraka na uhakika pamoja na kusaidia wageni wanaoingia nchini.
Aidha, alisema mfumo wa zamani ulikuwa na changamoto kubwa ikiwemo
kuzidiwa, kuwa na foleni kubwa hasa mwisho wa mwezi na kushindwa kutoa
huduma nyengine za kibenki za kimataifa kama viza na master card ambapo
kulikuwa kunatoa taswira mbaya kwa nchi.
Aibainisha kuwa, hivi sasa benki hiyo imepata mafanikio kwa kupata
faida kila mwaka kutoka mtaji usiofikia shilingi bilioni 1 kwa mwaka
2006 hadi mtaji ghafi wa shilingi 88 bilioni na mtaji wa msingi wa
shilingi 70 milioni.
Hivyo, aliishauri benki hiyo kuendelea kuchukua hatua ya kujiimarisha
na kuhimili zaidi ushindani wa kibiashara kwa taasisi nyengine za
kifedha ambao unazidi siku hadi siku.
Akizungumzia mapinduzi, alisema yameleta manufaa na mageuzi katika mfumo wote wa kijamii na kiuchumi.
Alisema Juni 30 mwaka 1966 serikali ilianzishwa rasmi benki ya watu
wa Zanzibar ambao ni uamuzi mwengine wa kimapinduzi wa kuimarisha huduma
za fedha na mikopo kwa wazanzibari.
Alisema, viongozi waliopo hivi sasa wataendelea kuiendeleza na kuidumisha ili lengo la kuanzishwa liendelee kudumu.
Alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wazanzibari kuendelea kuyalinda
mapinduzi yao na kutembea kifua mbele hasa katika miaka hii ambayo
inatimiza miaka 55.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, Juma Ameir Hafidh, alisema kutokana na
kukua kwa mfumo mpya wa teknolojia na mawasiliano, PBZ imefanya mageuzi
ya kubadilisha mfumo wa zamani na kuanzisha mfumo mpya kwa lengo la
kutoa huduma wakati wote.
Zanzibaleo.
Comments